Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matola aenda na Kapama

Matola Xkapama.jpeg Kapama ameanzishwa mchezo wa leo na Seleman Matola

Wed, 7 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Selemani Matola amefanya mabadiliko machache kwenye kikosi cha Simba kinachoanza mchezo wa mzunguko wa tatu wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC unaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mojawapo ya mabadiliko hayo ni kwenye eneo la kiungo ambalo amemuanzisha Nassoro Kapama ikiwa ni mechi yake ya kwanza ya ligi akiwa na kikosi hicho tangu aliposajiliwa kutoka Kagera Sugar.

Kwenye eneo la ushambuliji hakuna mabadiliko kwani litaendelea kuongozwa na Moses Phiri akisaidiana kwa ukaribu na viungo Pape Sakho na Augustine Okrah.

Matola anaongoza timu hii baada ya Klabu hiyo jana kutangaza kufikia makubaliano ya pande mbili ya kuachana na aliyekuwa kocha wake mkuu, Zoran Maki ikiwa ni miezi miwili tu tangu atangazwe kukinoa kikosi hicho akichukua nafasi ya Mhispania, Pablo Franco.

Kikosi kamili kinachoanza ni, Aishi Manula, Israel Mwenda, Mohamed Hussein 'Tshabalala', Henock Inonga, Mohammed Ouattara, Nassoro Kapama, Sadio Kanoute, Pape Sakho, Moses Phiri, Clatous Chama na Augustine Okrah.

Wachezaji wa akiba ni, Beno Kakolanya, Erasto Nyoni, Kennedy Juma, Mzamiru Yassin, Kibu Denis, Nelson Okwa, Dejan Georgijevic, John Bocco na Habibu Kyombo.

Mechi ya mwisho iliyopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa baina ya timu hizi Juni 19 mwaka huu, Simba ilishinda mabao 3-1 yaliyofungwa na Kibu Denis, Pape Sakho na Henock Inonga huku lile la KMC likifungwa na Hassan Kabunda aliyejiunga na Namungo msimu huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live