Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matola aanika kilichowaponza wakapigwa na Simba

Matola: Bado Tuna Matumaini Ya Kufanya Vizuri Ligi Kuu Matola aanika kilichowaponza wakapigwa na Simba

Sat, 20 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Yanga imeendeleza ubabe dhidi ya Simba msimu huu baada ya kuitandika mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu uliomalizika muda mchache uliopita Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Mabao ya Yanga katika mchezo huo yamefungwa na Aziz Ki dakika ya 19' kwa mkwaju wa penalti, bao la pili likifungwa na Joseph Guede dakika 39' akimpiga chenga hadi kipa, Ayoub Lakred.

Akizungumza baada ya mchezo huo kumalizika, Kocha Msaidizi wa Simba, Suleimani Matola ametaja sababu ya wao kupoteza mchezo huo kwa mara ya pili mfululizo kutoka kwa watani zao Yanga.

"Tulianza vizuri dakika za mwanzo na ndani ya dakika 10 za mwanzo tulipata nafasi za wazi lakini hatukufanikiwa kufunga. Kwa hiyo naweza kusema tatizo la wachezaji wetu kushindwa kutumia nafasi bado liko palepale.

"Tulifanya tactical sub baada ya Henock Inonga kuumia tukamuingiza Hussein Kazi lakini bahati mbaya dakika ya kwanza tu tangu aingie alifanya makosa, Yanga wakapata penati tukaadhibiwa bao la kwanza. Baadaye mabeki wakafanya kosa tena Yanga wakatuadhibu bao la pili.

"Tuliporudi kipindi cha pili tulibadilisha mpango tukafanya sub na kuanza kushambulia kwa kasi, bahati nzuri tukafanikiwa kupata bao moja lakini halikutosha na mwisho wa mchezo tukapoteza.

"Kuhusu ubingwa kwa sasa naweza kusema ni ngumu kuupata lakini tunaangalia zaidi mechi zilizosalia kuona tutapata nini," amesema Matola.

Mchezo wa mwisho walipokutana katika dabi ya Kariakoo Novemba 05, 2023 Simba SC walifungwa 5-1. Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha alama 58 baada ya michezo 22 huku Simba wakisalia na alama 46 kwenye nafasi ya tatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live