Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matola: Tunajiandaa kupata ushindi

Matola: Bado Tuna Matumaini Ya Kufanya Vizuri Ligi Kuu Kocha. Msaidizi Simba SC, Seleman Matola

Thu, 18 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Msaidizi Simba SC, Seleman Matola amesema kuwa wanajiandaa kupata ushindi mbele ya wapinzani wao, Yanga kuelekea kwenye mchezo wa dabi utakaopigwa Jumamosi Aprili 20, 2024.

Matola amesema hayo wakati akizungumzia maandalizi ya kikosi chake ambacho kimekita kambi Zanzibar kuelekea mchezo huo mkubwa Barani Afrika.

“Wachezaji wapo fiti na wana morali ya kutosha kwa mchezo huo kwani lengo letu ni kupata ushindi. Benchi la ufundi linaendelea kurekebisha mapungufu ili timu iwe na makali ya hali ya juu.

"Hatukuwa na matokeo mazuri katika mechi zilizopita zilizopita lakini hatutakubali kupoteza katika mechi zetu zijazo hasa katika mchezo na Young Africans, tunahitaji kupata ushindi,” amesema Matola.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live