Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matola: Msimu ujao tutawafunga sana

Matola: Bado Tuna Matumaini Ya Kufanya Vizuri Ligi Kuu Matola: Msimu ujao tutawafunga sana

Thu, 18 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha msaidizi wa Simba, Seleman Matola ameeleza kuwa tatizo la ufungaji limepata mwarobaini baada ya kocha mkuu wa timu hiyo, Fadlu Davids kuwapa washambuliaji Program maalum ya namna ya kufunga kwa ajili ya msimu mpya wa 2024/25.

Amesema msimu uliopita hawakufanya vizuri sana kwenye safu hiyo na kushindwa kufikia malengo yao ya kutwaa ubingwa na kuishia kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Simba msimu uliopita wa 2023/24 walifunga jumla ya mabao 59 na kufungwa 25 tofauti na 2022/23 ambao walifunga mabao 75 na kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara 17, kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kazi kubwa ambayo anaifanya Kocha Fadlu ni kuwapa mbinu washambuliaji wakiongozwa na Kibu Denis, Freddy Michael, Steven Mukwala na Joshua Mutale mwenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani.

Matola ameiambia Spotileo kuwa kocha Fadlu anapita katika njia ya Simba ambao makocha waliofanikiwa kipindi cha timu hiyo ilipofanikiwa na tangu amekabidhiwa anasisitiza zaidi washambuliaji kuwa makini wanapokuwa uwanjani.

“Ufungaji ndio kazi kubwa anayoifanya, licha ya kutaka mpira uchezwa lakini amekuwa makini kwenye ufungaji na mabeki, baada ya kuona tathimini ya misimu miwili ya ligi kuona tulipopanda na kushuka,” amesema Matola.

Kuhusu usajili wa vijana, Matola amesema wameangalia zaidi vipaji na uwezo wa wachezaji waliosajiliwa, kocha Fadlu kazi yake imekuwa rahisi kuweka katika mfumo wa Simba ambao wamezoeleka.

Simba inaendelea kujifua nchini Misri katika mji wa Ismailia walipoweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya wa mashindano ya Ligi Kuu Bara na michuano ya kombe la Shirikisho Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: