Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matola: Kwa hali hii, ubingwa ni ngumu

Selemani Matola Matola: Kwa hali hii, ubingwa ni ngumu

Sat, 20 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha msaidizi wa Simba Seleman Matola amesema kwasasa mbio za ubingwa ni ngumu kwao lakini watapambana kumaliza vyema michezo iliyosalia.

Akizungumza baada ya mchezo dhidi ya Yanga uliomalizika kwa vijana wake kuvurugwa 2-1 kocha huyo amesema bado shida yao ya kushindwa kutumia nafasi inawatafuna.

"Kuhusu ubingwa kwa sasa naweza kusema ni ngumu kuupata lakini tunaangalia zaidi mechi zilizosalia kuona tutapata nini," amesema Matola.

Mchezo wa mwisho walipokutana katika dabi ya Kariakoo Novemba 05, 2023 Simba SC walifungwa 5-1. Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha alama 58 baada ya michezo 22 huku Simba wakisalia na alama 46 kwenye nafasi ya tatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live