Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matola: Gari la Chama bado halijawaka

Bwalya Chama Matola: Gari la Chama bado halijawaka

Sun, 6 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KOCHA Msaidizi wa Simba, Seleman Matola amefungukia kiwango cha kiungo wa timu hiyo, Clatous Chama na kudai kuwa bado anajitafuta.

Matola amesema kuwa Chama bado hajafikia kwenye kile kiwango chake ambacho aliondoka nacho, ingawa amekuwa akicheza vizuri kwenye mechi ambazo amepewa nafasi.

Matola alisema, Chama hakucheza kwa muda mrefu na ndiyo maana amekuwa akipanda kiwango chake taratibu, ila itafika wakati atakuwa kama vile alivyokuwa zamani.

“Chama bado hajafikia kwenye kiwango chake ambacho aliondoka nacho, ingawa amekuwa akicheza vizuri, inatakiwa tuendelee kumpa muda.

“Tumekuwa tukimlinda pia ili asiweze kuumia kutokana na kutocheza muda mrefu na ndiyo maana kwenye mechi zote hajacheza kwa dakika 90,” alisema Matola.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live