Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matola: Asec MiMosas hawatoboi kwa Mkapa

Simba SC 1140x640 Asec MiMosas hawatoboi kwa Mkapa

Fri, 4 Feb 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola anakiri mechi yao ya kwanza ya Kundi D ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast sio nyepesi, lakini amewahakikisha wanasimba kwamba wapinzani wao hao hawatatoboa Dar.

Matola anaijua vyema Asec kwani mwaka 2003 akiwa mchezaji alishakutana nao katika mechi za makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kudai sio timu ya kubezwa, lakini wao kama Simba wamejipanga kuhakikisha wanaanza vyema.

Februari 13, Simba itakuwa mwenyeji wa Asec katika mechi itakayopigwa kuanzia saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam na Matola alisema anawakumbuka wapinzani hao, pia sio wa kubeza kutokana na uwezo wao.

Alisema, wameanza kuwafuatilia kwa kutazama video zao mbalimbali za ndani na nje katika mechi zao mbalimbali ili kubaini namna gani ya kuwakabili.

Matola alisema, kwa sasa wamepata muda mchache wa kuwatazama kwa vile akili zao zimeelekezwa katika mchezo wa leo dhidi ya Tanzania Prisons na ule ya Jumpili dhidi ya Mbeya Kwanza.

“Huo mchezo wetu wa kimataifa ni muhimu sana, kwani tunataka tuanze vyema mechi za makundi, lakini kwa sasa tunatolea macho yetu michezo ya ligi,” alisema Matola aliyeongeza kuwa baada ya mechi ya Jumapili ndipo watajikita kuichabo Asec.

Katika mechi yao ya mwaka 2003, Asec ilipasuka Dar kwa bao 1-0 kisha kwenda kushinda kwao kwa mabao 4-3 na Matola alifafanua; “Hawa jamaa ni wazuri sana, ni mchezo utakaokuwa na ushindani, ila tunaamini tutashinda kwa maandalizi tunayoendelea nayo.”

Simba imeangukia Kombe la Shirikisho baada ya kuondoshwa Ligi ya Mabingwa Afrika na Jwaneng Galaxy ya Botswana kwa faida ya mabao ya ugenini baada ya sare ya 3-3, Simba ikishinda ugenini 2-0 na kulala 3-1 Dar.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz