Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matokeo ya dabi yanaamuliwa kwa nje ya uwanja - Boniface Jacob

Simba X Yanga CAF Matokeo ya dabi yanaamuliwa kwa nje ya uwanja - Boniface Jacob

Wed, 17 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meya wa zamani wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amesema kuwa matokeo ya mchezo wa dabi kati ya Simba na Yanga hayaamuliwi kwa ubora wa timu ndani ya uwanja bali ujanja nje ya uwanja.

Jacob ambaye ni shabiki wa Simba amesema hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X zamani Twitter kuelekea mchezo wa hayo kuelekea mchezo wa dabi utakaopigwa Aprili 20.

"Kwa sisi tulio zaliwa Dar es Salaam na kukulia Dar es Salaam kuna utamaduni wa siku nyingi sana kuhusu Kariakoo Derby. Timu ambayo ni mbovu na dhaifu sana katika msimu huo, iwe Simba au Yanga ndiyo timu yenye uhakika wa ushindi kwa 96%.

"Mfano Simba tulipochukua ubingwa mara 4 mfululizo, Simba ikiwa ya moto, lakini tuliwafunga Yanga mara moja tu Kati ya mechi 10+.

"Kwa siri hii, ewe mwana Simba hupaswi kuhofi kwenda Uwanjani. Matokeo ya Kariakoo Derby hayaamuliwi kwa ufundi au kikosi bora bali uchawi, fitina, mizengwe na jitihada za nje ya uwanja. Mimi nitaenda uwanjani," amesema Boniface Jacob.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live