Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matokeo Uchaguzi Bodi ya Ligi hadharani

Tplb Matokeo ya Uchaguzi Bodi ya Ligi

Fri, 3 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Azam FC, Nassor Idrisa 'Father' ameshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TPLB) katika uchaguzi uliofanyika leo hoteli ya Cate mjini Morogoro.

Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Jarvis Mnguto amefanikiwa kutetea nafasi yake ya Uenyekiti wa Bodi kwa awamu nyingine tena tangu ampokee kijiti aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga mwaka 2018.

Ikumbukwe Kamati ya Uchaguzi ya TFF, chini ya Mwenyekiti, Wakili Kiomoni Kibamba iliwaengua Mwenyekiti wa Yanga SC, Dk Mshindo Mbette Msolla na wa Simba SC, Murtaza Ally Mangungu kwa sababu tofauti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live