Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matheo kuikosa Geita

MATHEO ANTHONY INJ Matheo kuikosa Geita

Wed, 9 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Mshambuliaji Matheo Anthony wa KMC ataukosa mchezo wao ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Geita utakaochezwa Ijumaa katika uwanja wa Nyankumbu, Geita.

Matheo mwenye mabao manne aliumia kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Kagera Sugar ambao ulimalizika huku wakifungwa 1-0.

Akizungumza Kocha mkuu wa KMC, Thiery Hitimana alisema kwenye mchezo huo atamkosa mshambuliaji wake hatari Matheo (Anthony) ambaye hali yake bado haijawa vizuri.

Hitimana alisema licha ya kukosekana kwa mchezaji huyo atamkosa kiungo wake Awesu Awesu huku akimtazamia beki wake Ibrahim Ame hali yake itakavyokuwa.

"Wachezaji wote hawa ni wa kwenye kikosi cha kwanza kwahiyo kuna pigo fulani lakini tuna wachezaji 25 ambao wote ni wa kwenye timu yetu hivyo wapo wengine wa kucheza,"alisema Hitimana.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo husika, Hitimana alisema wanaendelea na maandalizi na bado wana siku nyingi za kukisuka kikosi chao.

"Tuna siku nyingi hadi Ijumaa kwa ajili ya mchezo wenyewe, kikosi kina hali nzuri na mazoezi yanaendelea."

KMC inashika nafasi ya tisa ikiwa na pointi 13 kwenye msimamo wa Ligi huku ikicheza mechi 10 imeshinda tatu, sare nne na kupoteza mechi tatu.

Chanzo: Mwanaspoti