Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Materazzi: Sijaonana na Zidane tangu anipige kichwa

Materazzi X Zidane Materazzi: Sijaonana na Zidane tangu anipige kichwa

Tue, 2 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa zamani wa timu ya taifa ya Italia, Marco Materazzi, amesema tangu alipopigwa kichwa na Zinedine Zidane mwaka 2006, hajaonana na staa huyo.

Tukio hilo lilitokea kwenye fainali ya Kombe la dunia ambapo Ufaransa walicheza dhidi ya Italia. Wawili hao walionekana kupishana kauli ndipo Zidane alimgonga kichwa beki huyo wakati mchezo unaendelea na akaoneshwa kadi nyekundu.

“Nakumbuka tulikuwa kwenye marumbano na matusi ndani yake wakati mchezo unaendelea, mwisho wa siku akaniambia atanipa jezi yake, hapo ndipo nikakataa na kumwambia ningependa anipe dada yake, ndipo akageuka na kunipiga kichwa. Tangu tukio hilo litokee hadi leo sijaonana na Zidane.” Alisema Materazzi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live