Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matawi kuchagua Viongozi Yanga SC

MASHABIKI YANGA Matawi kuchagua Viongozi Yanga SC

Mon, 14 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga itafanya Uchaguzi wa viongozi wapya mwishoni mwa mwezi Juni 2022, ikiwa ni matakwa ya katiba mpya ya klabu hiyo ambayo inawataka kufanya hivyo ndani ya kipindi hiki.

Ambapo watachagua Rais wa klabu, Makamu wa Rais na sio Mwenyekiti tena kama ilivyokwa hapo awali.

Lakini pia wameweka wazi kuwa watafanya mabadiliko ya wapiga kura kwa sasa viongozi wa matawi ndio watakaochagua viongozi kwenye uchaguzi mkuu na sio wanachama hai wote wenye kadi kama ilivyokuwa hapo awali.

Wapiga Kura hao ni kutoka kwenye matawi ambapo ni Mwenyekiti, Khatibu, Mtunza fedha na Wajumbe wawili (Mmoja akiwa Mwanamke kama yupo).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live