Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matampi awapa jeuri Coastal Union

Ley Matampi Ley Matampi.

Fri, 23 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati golikipa tegemeo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Ley Matampi, akirejea kikosini, Coastal Union imeahidi kupata ushindi mnono katika mechi ya marudiano ya michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bravos Do Maquis itakayochezwa Jumapili.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, David Ouma, alisema jana kurejea kwa Matampi kumewapa nguvu ya kupambana kupata ushindi ambao utawafanya wasonge mbele katika michuano hiyo.

Ikiwa ugenini nchini Angola, Coastal Union, ilibugizwa mabao 3-0 na hivyo inahitaji ushindi wa kuanzia magoli 4-0 katika mchezo wa marudiano utakaochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam ili isonge mbele.

Kocha huyo alitaja sababu mbalimbali ambazo zilisababisha kupoteza mechi ya kwanza ikiwamo baadhi ya wachezaji wake kuwa majeruhi.

"Hatujakata tamaa, tulifungwa mabao 3-0, tulikuwa ugenini lakini safari hii tutakuwa nyumbani, tunacheza mbele ya mashabiki wetu pamoja na hali ya hewa tuliyoizoea, moja ya vitu ambavyo vilitukwaza ni hali ya hewa, nao pia kwetu wataathirika nalo, ilikuwa baridi kwetu itakuwa ni joto kwao, hivyo tutaitumia faida hiyo kupindua meza," alisema Ouma.

Mchezaji Jackson Shiga, naye alisema urejeo wa Matampi langoni, imeamsha ari ya wachezaji kupambana kwani wanajua uwezo wake na jinsi aliyowabeba msimu uliopita.

"Tumerudi nyumbani, mchezo hautakuwa rahisi wala mgumu, kikubwa ni kupata matokeo mazuri na kusonga mbele, kinachotupa nguvu ya kusema hivi ni urejeo wa Matampi, alikuwa na matatizo ya hapa na pale, kila mtu sasa ana imani na kuona mchezo wa Jumapili utakuwa bora sana kwetu," alisema Shiga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live