Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matampi aikingia kifua Coastal

Coastal Union Wamkanda Mtu 4 0 Wamtambia Simba 'anayefuata Ajiandae' Matampi aikingia kifua Coastal

Sun, 8 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Msaidizi wa Coastal Union, Fikiri Elias amemtetea kipa wa timu hiyo, Ley Matampi aliyesababisha bao pekee lililoipa ushindi Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyopigwa Mkwakwani jijini Tanga na kuwafanya wageni hao kupanda hadi kileleni mwa msimamo .

Katika mechi hiyo, Matampi alishindwa kuupiga mbali mpira aliouparaza baada ya kuchimba chini, hivyo kumfanya Kipre Junior auwahi na kutoa pasi ya haraka kwa Feisal Salum aliyefunga bao hilo la ushindi, lakini kocha Elias alisema walikosa bahati juzi usiku na wala hana wa kumlaumu akiwamo kipa huyo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Fikiri alisema haikuwa bahati yao katika mchezo huo kwani wachezaji walijituma na kufuata maelekezo waliyowapa ipasavyo hivyo hakuna mchezaji wa kumlaumu kwani makosa humtokea yeyote.

“Makosa kwenye mpira ni jambo la kawaida hivyo kilichotokea tumekubaliana nacho na tunarudi kujipanga tena kuangalia ni wapi tumekosea ili turekebishe kwa lengo la kurudi tukiwa imara zaidi ya sasa hivi,” alisema Fikirini.

Kocha huyo, alisema kwa vile kuna wiki tatu ambazo kikosi hicho hakitacheza watatumia kutafuta michezo ya kirafiki kwa lengo la kujiweka fiti kabla ya kurudi tena kwenye muendelezo wa Ligi Oktoba 26 kuivaa Ihefu.

Matampi mwenye uzoefu mkubwa, akiidakika timu ya taifa ya DR Congo katika fainali za Kombe la Afrika (Afcon) 2019 huo ulikuwa mchezo wake wa kwanza kuanza akiwa na kikosi hicho tangu alipojiunga na Coastal Union kutoka AS Renaissance aliyokuwa akiichezea mbali na TP Mazembe, DC Motema Pembe na FC Lupopo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live