Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastraika wenye dawa ya kutibu maradhi ya Arsenal, Manchester United

Jonathan David Pwm Jonathan David

Fri, 12 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Arsenal na Manchester United kwa siku za karibuni zimekuwa zikitaabika uwanjani kutokana na mastraika wao kushindwa kufunga mabao licha ya kutengenezewa nafasi nyingi.

Arsenal ilipiga mashuti 48 kwenye mechi mbili zilizopita bila ya kufunga baada ya Gabriel Jesus, Kai Havertz na Eddie Nketiah kushindwa kutimiza wajibu wao sawasawa.

Wapinzani wao, Man United, nako mambo si shwari. Miamba hiyo ya Old Trafford imefunga mabao 22 tu kwenye Ligi Kuu England msimu huu, ikiwa ni idadi ndogo kushinda hata kwa timu inayoshika nafasi ya 17 kwenye msimamo, Everton (24) na timu inayoshika nafasi ya 18, Luton (23).

Washambuliaji Marcus Rashford na Rasmus Hojlund wamekosa nafasi nyingi sana katika mechi ya raundi ya tatu ya Kombe la FA dhidi ya Wigan, Jumatatu iliyopita.

Hilo linathibitisha kwamba Man United na Arsenal zote zimekuwa na matatizo ya washambuliaji. Kitu kizuri hilo limetokea wakati dirisha la usajili wa mastaa la Januari likiwa wazi, hivyo kazi ni kwao.

Kwa shida hiyo ya ukosefu wa mabao unaozikabili Arsenal na Man United, hawa hapa mastraika wa kwenda kutibu maradhi yao na kuwapa raha mashabiki kwa kushangilia mabao.

VICTOR BONIFACE

KLABU: Bayer Leverkusen

UMRI: 23

BEI YAKE: Pauni 50milioni

Tangu alipojiunga na Bayer Leverkusen kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi akitokea Union Saint-Gilloise ya Ubelgiji kwa ada ya Pauni 17 milioni, straika huyo Mnigeria amekuwa moto uwanjani.

Akiwa chini ya Kocha Xabi Alonso, Bonifave ameifanya Leverkusen kutamba kwenye Bundesliga ikiongoza kwenye msimamo, huku akiwa amefunga mabao 16 katika mechi 23 za michuano yote.

Ada yake ya uhamisho inaweza kuwa kati ya Pauni 40 milioni na Pauni 50 milioni, hiyo inatosha kumng’oa kwenye timu hiyo, licha ya Leverkusen kutazamiwa kuwa wagumu kutokana na ubora wa mchezaji huyo, hasa kutokana na kuwa na mkataba mrefu, miaka minne.

SANTIAGO GIMENEZ

KLABU: Feyenoord

UMRI: 22

BEI YAKE: Pauni 60milioni

Mmoja kati ya washambuliaji matata kabisa kwenye soka la Ulaya kwa sasa, ambapo Muargentina huyo ukimtaka, basi weka mezani Pauni 60 milioni.

Feyenoord itapambana sana kubaki na mshambuliaji huyo, ambaye aliwapa ubingwa wa Eredivisie msimu uliopita baada ya kufunga mabao 15 katika mechi 32 za ligi. Na tayari msimu huu ameongoza kwa mabao baada ya kufunga mara 18 katika mechi 16, akiweka pia Feyenoord kwenye nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, ikiwa pointi 10 nyuma ya vinara wa ligi ya Uholanzi, PSV. Kiwango cha Gimenez bila ya shaka kitafanya timu nyingi za Ulaya kwenda kunasa saini yake haraka.

JONATHAN DAVID

KLABU: Lille

UMRI: 23

BEI YAKE: Pauni 40milioni

Mkataba wake umebakiza muda usiozidi miezi 18 huko kwenye kikosi cha Lille ya Ufaransa, hiyo ina maana mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Canada hana muda mrefu wa kuendelea kubaki kwenye kikosi hicho.

Huduma yake inaweza kupatikana kwa ada kati ya Pauni 30 milioni hadi Pauni 40 milioni, kiwango ambacho kuna timu nyingi inaweza kulipa na kunasa saini yake ili akacheze kwenye vikosi vyao.

David alijiunga na Lille mwaka 2020 akitokea Gent ya Ubelgiji na amefunga mabao 13 kwenye Ligue 1, alipoisaidia Lille kushinda ubingwa wa Ligue 1. Baada ya kiwango bora msimu wa 2022/23, alipofunga mabao 24 katika mechi 37 za ligi, amekuwa gumzo kubwa Ulaya, huku msimu huu amefunga matano hadi sasa.

SERHOU GUIRASSY

KLABU: Stuttgart

UMRI: 27

BEKI YAKE: Pauni 15milioni

Mshambuliaji huyo wa Guinea yupo kwenye miaka ya kucheza soka bora uwanjani, ambapo huko kwenye Bundesliga amefunga mabao 17 katika mechi 14 alicheza msimu huu. Na kama asingepata maumivu ya misuli Oktoba mwaka jana, basi idadi yake ya mabao ingekuwa kubwa zaidi.

Alivunja rekodi ya Robert Lewandowski ya mabao kwenye Bundesliga baada ya kufunga mara 13 kwenye mechi saba za mwanzo. Licha ya kiwango hicho matata kabisa huko Stuttgart, fowadi huo kwenye mkataba wake kumewekwa kipengele kinachohitaji ilipwe Pauni 15 milioni tu kwa timu itakayohitaji huduma yake. Kasi yake hiyo ya ufungaji na bei anayouzwa, timu itakayofanikiwa kumsajili, itakuwa imepiga bao.

DUSAN VLAHOVIC

KLABU: Juventus

UMRI: 23

BEI YAKE: Pauni 50milioni

Straika ambaye Arsenal ilishindwa kumsajili Januari 2022, Vlahovic amerejea tena kwenye orodha hiyo. Mwaka huo, mkali huyo aliyesajiliwa na Juventus kwa ada ya jumla ya Pauni 70 milioni.

Vlahovic alikubwa na maumivu ya misimu miezi 12 iliyopita na hilo lilitibua kasi yake kwenye kufunga mabao na ndiyo maana thamani yake pia imeshuka hadi kufikia Pauni 50 milioni. Bado ni mchezaji mwenye uwezo wa kufunga, ametikisa nyavu mara 24 katika mechi 59 za ligi.

Hata hivyo, Kocha Mikel Arteta bado anavutiwa na mchezaji huyo na huenda akahangaika kunasa huduma yake kwenda kumpunguzia stresi za kukosa mabao. Mkataba wake huko Juventus unafika mwisho Juni 2026.

TEREM MOFFI

KLABU: Nice

UMRI: 24

BEI YAKE: Pauni 25milioni

Kwa sasa yupo zake Afcon 2023 akiwa na kikosi cha Nigeria, Moffi anatarajia kurejea kwenye klabu yake akiwa kwenye afya njema kwa sababu lolote linaweza kutokea kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi. West Ham United ilijaribu kumsajili Januari mwaka jana kwa ada ya Pauni 25 milioni na thamani yake imeongezeka kidogo baada ya kufunga mabao sita katika mechi 16 alizocheza Ligue 1 tangu alipojiunga jumla na Nice wakati wa dirisha lililopita la majira ya kiangazi.

Alitengeneza jina lake Lorient alikofunga mabao 34 kwenye ligi baada ya misimu miwili na nusu na alisaidia Nice kushika namba mbili, pointi tano nyuma ya vinara PSG.

LOIS OPENDA

KLABU: RB Leipzig

UMRI: 23

BEI YAKE: Pauni 70milioni

Ni Guirassy na Harry Kane ndiyo pekee waliofunga mabao mengi kwenye Bundesliga msimu huu, huku Openda na mabao yake 11 amekuwa akizuvutia timu nyingi za Ulaya kuhitaji saini yake.

Alijiunga na Leipzig kwa ada ya Pauni 40 milioni kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi akitokea Ufaransa, ambako alifunga mabao 21 katika mechi 38 za Ligue 1. Mabao mawili aliyofunga Etihad kwenye kichapo cha mabao 3-2 cha Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City. Alionyesha kile Openda anachoweza kufanya uwanjani. Akiwa na mkataba wa miaka minne na nusu, Openda amewekewa kipengele kinachohitaji kulipwa Pauni 70 milioni tu kuvunjwa.

Chanzo: Mwanaspoti