Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastraika wa kurudisha furaha Darajani ni hawa

Osimhen 1280x720.jpeg Mastraika wa kurudisha furaha Darajani ni hawa

Fri, 21 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ubutu wa safu ya ushambuliaji ya Chelsea umewagharimu dhidi ya Real Madrid na kujikuta wakitupwa nje ya mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa juzi Jumanne.

The Blues imetupwa nje kwenye michuano hiyo ya Ulaya, hatua ya robo fainali huku ikishindwa kufunga hata bao moja dhidi ya mabingwa hao wa tetezi, Real Madrid - ambao walishinda 2-0 nyumbani na ugenini hivyo kusonga mbele kwa jumla ya mabao 4-0.

Katika mechi ya marudiano iliyofanyika Stamford Bridge, wachezaji kama Marc Cucurella na N’Golo Kante walipoteza nafasi muhimu kabisa za kufunga ambazo zingerudisha uhai Chelsea.

Na sasa straika mpya utakuwa mjadala muhimu kwa bilionea Todd Boehly kuhakikisha anapata mmoja kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi. Licha ya kutumia Pauni 600 milioni, kinara wa mabao Chelsea ni Namba 10 wao, Kai Havertz mwenye mabao tisa.

Mastraika wao waliopo kwenye kikosi Pierre-Emerick Aubameyang na Armando Broja, wamefunga mabao manne tu kati yao. Hata, Romelu Lukaku - aliyefunga mabao 15 msimu uliopita alikuwa na afadhali. Sawa, Christopher Nkunku, aliyefunga mabao 17 msimu huu na 35 uliopita, atatua Stamford Bridge mwishoni mwa msimu huu.

Na huenda wakamchukua jumla pia Joao Felix, licha ya Mreno huyo kufunga mara mbili tu tangu aliponaswa kwa mkopo kwenye dirisha la Januari akitokea Atletico Madrid.

Lakini, linapokuja suala la kutaka Namba 9 asilia, Chelsea inahitaji kuingia sokoni. Na kutokana na hilo, hii hapa orodha ya mastraika ambao Chelsea inawahitaji kuja kuokoa jahazi.

HARRY KANE — TOTTENHAM Nahodha wa England, Harry Kane 29, anaonekana yupo kwenye mpango wa kuachana na klabu yake hiyo ya ujanani mwishoni mwa msimu huu. Tottenham imeshindwa kubeba taji chini ya Antonio Conte na haionekani kuwa na nguvu hiyo kwa msimu huu.

Kane yeye amethibitisha kwamba ni mfungaji mahiri wa mabao, akifunga mara 273 kwa Spurs na 55 kwa timu ya taifa.

Uhamisho wa Stamford Bridge utachochea zaidi upinzani wa klabu za Spurs na Chelsea, ambazo zote zipo London. Mkataba wa Kane utakwisha 2024 na tajiri Boehly anaweza kufanya jambo.

ALSO READ Ubingwa ulivyopinduliwa dakika za mwisho England Spoti Majuu 54 min ago

VICTOR OSIMHEN — NAPOLI Straika wa Kinigeria, Victor Osimhen, 24, ni mchezaji atakayeshindaniwa sana kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Staa huyo amefunga mabao 26 huko Napoli msimu huu na ameiongoza timu hiyo kuwa kwenye wakati mzuri wa kubeba taji lao la kwanza la Serie A tangu mwaka 1990.

Osimhen hajaweka kificho juu ya ndoto zake za kwenda kucheza Ligi Kuu England, huku shujaa wake, Didier Drogba - aliwahi kucheza Chelsea. Tajiri wa Chelsea, Boehly kwa sababau si mgumu wa kutoa pesa anaweza kunasa saini ya Osimhen.

IVAN TONEY — BRENTFORD Straika huyo Mwingereza, Ivan Toney amekuwa na wakati mzuri kabisa kwenye kikosi cha Brentford msimu huu. Toney, 27, ametumikia miaka saba ya kucheza kwenye League One kabla ya Brentford kumchukua kwenye Championship na sasa wanacheza Ligi Kuu England.

Amefunga mabao 66 katika kipindi kisichofika miaka mitatu akiwa na Brentford, ikiwamo mabao 19 ya msimu huu. Toney ana nguvu na ufundi na kuwa wa staili ileile ya washambuliaji Namba 9 ambao wamekuwa wakihusudiwa na Chelsea.

MARCUS THURAM — EINTRACHT FRANKFURT Mtoto wa gwiji wa Ufaransa, Lillian Thuram, Marcus amefunga mabao 16 msimu huu akiwa na kikosi cha Frankfurt.

Ana uwezo wa kucheza kama straika au winga na amekuwa mtu muhimu kwenye kikosi cha Ufaransa kwa siku za karibuni.

Thuram, 25, amekuwa akionyesha ubora mkubwa kila msimu na kitu kizuri ni kwamba mwishoni mwa msimu huu anaweza kupatikana bure kutokana na mkataba wake Frankfurt kufika tamati Juni mwaka huu. Manchester United, Tottenham, Newcastle, Juventus na Inter Milan zinamtaka pia mshambuliaji huyo.

RANDAL KOLO MUANI — EINTRACHT FRANKFURT Mshambuliaji mwingine wa Frankfurt, ambaye amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu.

Muani, 24, amejitengeneza na kuelekea kuwa mshambuliaji mahiri Ulaya baada ya kufunga mabao 20 katika msimu wake wa kwanza akiwa na miamba hiyo ya Ujerumani. Kama Thuram, naye amekuwa muhimu kwenye kikosi cha Ufaransa chini ya Didier Deschamps.

Ameripotiwa kuwa kwenye mpango pia wa kocha Thomas Tuchel, akitaka akakipige Bayern Munich. Kolo Muani atakuwa ingizo muhimu akitua zake Chelsea kutokana na ubora wake.

OLLIE WATKINS — ASTON VILLA Straika zamani wa Brentford, Ollie Watkins, 27, amekuwa moto kwelikweli tangu zilipomalizika fainali za Kombe la Dunia 2022 huko Qatar. Staa huyo amefunga mabao 14 kwenye Ligi Kuu England akiwa na kikosi cha Aston Villa.

Baada ya kuhamishiwa kwenye nafasi ya mshambuliaji wa kati, Watkins amekisaidia kikosi hicho kinachonolewa na Mhispaniola, Unai Emery kufanya kweli kwenye ligi na sasa inafukuzia nafasi ya kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao. Watkins atakuwa na msaada mkubwa kwenye kikosi cha Chelsea kama atanaswa.

FOLARIN BALOGUN — ARSENAL Vitu vya kushangaza vinatokea kwenye soka, lakini Folarin Balogun anaweza kuwa mmoja wa mastraika ambao Chelsea inaweza kuwachukua kwenda kufanya mambo kuwa mepesi Stamford Bridge. Balogun, 21, amekuwa moto huko Ligue 1 anakocheza kwa mkopo Reims baada ya kufunga mabao 18.

Kwenye ligi hiyo ya Ufaransa, Balogun amewafanyia maajabu mastaa matata kabisa kama Lionel Messi na Kylian Mbappe katika ishu ya kufunga mabao, hivyo Chelsea watakuwa kwenye mikono salama wakimchukua staa huyo wa Arsenal.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: