Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastraika wa bei ghali Ligi Kuu England

Haaland Hat Trick Erling Haaland

Fri, 22 Sep 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mambo ni moto. Ligi Kuu England imejaa mastaa kibao wa eneo la ushambuliaji hasa baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili. Klabu kibao zimetumia pesa nyingi kwenye dirisha la usajili na kutengeneza safu matata kabisa za ushambuliaji kwa ajili ya mikikimikiki ya Ligi Kuu England msimu huu.

Lakini, je, washambuliaji hao kwa sasa wana thamani kiasi gani? Kwa mujibu wa Football Observatory, hii hapa orodha ya washambuliaji wenye thamani kubwa zaidi kwenye Ligi Kuu England msimu huu. Mambo ni moto.

10. Gabriel Jesus - Arsenal (Pauni 68.9 milioni)

Mbrazili huyo ni miongoni mwa mastraika bora kwenye orodha Ulaya, alijiunga na Arsenal akitokea Manchester City mwaka jana baada ya kubeba mataji manne ya Ligi Kuu England na mataji matatu ya FA. Jesus ana thamani ya Pauni 68.9 milioni na ndiye fowadi mkongwe kwenye orodha hii. Fowadi huyo alikosa mechi za mwanzo msimu ulipoanza kutokana na majeraha lakini alifunga mabao 11 na kutoa asisti sita msimu uliopita licha ya kusumbuliwa na majeraha.

9. Alexander Isak - Newcastle (Pauni 68.9 milioni)

Isak alijiunga na Newcastle msimu uliopita akitokea Real Sociedad. Straika huyo wa kimataifa wa Sweden alianza kwa kishindo St James Park kwani alifunga mabao 10 msimu uliopita. Straika huyo alifunga bao moja katika ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Aston Villa kwenye mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu msimu huu.

8. Moussa Diaby - Aston Villa (Pauni 68.9 milioni)

Diaby alijiunga na Aston Villa kwenye usajili wa dirisha la kiangazi akitokea Bayer Leverkusen na tayari ameorodheshwa kwenye orodha ya mastraika ghali zaidi Ligi Kuu England. Straika huyo wa kimataifa wa Ufaransa thamani yake inafanana na Isak na Jesus kwani walinunuliwa kwa Pauni 68.9 milioni. Mpaka sasa straika huyo amefunga mabao mawili na kutoa asisti mbili katika mechi tano alizocheza.

7. Antony - Man Utd (Pauni 68.9 milioni)

Winga huyo amesuasua tangu alipotu na Manchester United akitokea Ajax, licha ya kununuliwa kwa mkwanja mrefu kiwango chake bado hakijaridhisha. Kwa sasa winga huyo anakabiliwa na shutma za kumpiga na kumjeruhi mpenzi wake wa zamani Gabriela Cavallini. Msimu uliopita hakuwa na mwanzo mzuri kwani alifunga mabao manne tu kwenye ligi.

6. Cody Gakpo - Liverpool (Pauni 68.9m)

Gakpo ni usajili mpya wa Liverpool thamani yake imefanana na hela alionunuliwa Jesus, Antony, Isak na Diaby. Fowadi huyo alihusishwa na Man United kwenye usajili lakini Liverpool ikapindua meza na kumnasa. Gakpo amekuwa na mchango kwenye safu ya ushambuliji na tayari amefungua akaunti yake mabao kwenye ushindi wa mabao 3-1 dhidi Wolves msimu huu.

5. Darwin Nunez - Liverpool (Pauni 86.2 milioni)

Nunez alitua Liverpool lakini ameshindwa kupenya katika kikosi cha kwanza mbele ya Mohamed Salah mwenye umri wa miaka 31. Ingawa Nunez bado anaendelea kusuasua Anfield tangu aliponunuliwa kwa Pauni 85 milioni akitokea Benfica, fowadi huyo wa kimataifa wa Uruguay ameonyesha kiwango kizuri hivi karibuni dhidi ya Newcastle kwani alifunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 2-1 mwezi

4. Marcus Rashford - Man Utd (Pauni 86.2 mil)

Rashford alisaini mkataba mnono kufuatia mchango mkubwa aliotoa kwa timu yake msimu uliopita. Straika huyo alifunga mabao 17 na kutoa asisti tano kwenye ligi, lakini licha ya kuanza vibaya tayari amefungua akaunti yake ya mabao na amepania kuendeleza ubora wake katika mashindano mbalimbali msimu huu.

3. Julian Alvarez - Man City (Pauni 86.2 milioni)

Licha ya kukosa nafasi ya kudumu kikosi cha kwanza msimu uliopita sasa Pep Guardiola ameanza kumuamini kwani amempanga kila mechi tangu msimu ulipoanza. Fowadi huyo alibeba ubingwa wa Kombe la Dunia akiwa na umri wa miaka 23, pia alifunga mabao 17 msimu uliopita na tayari amefunga mabao mawili na kutoa asisti tatu msimu huu.

2. Gabriel Martinelli - Arsenal (Pauni 129.3m)

Baada ya kusaini mkataba mrefu na Arsenal mapema mwaka huu, Martinelli thamani yake ilipanda na kufika Pauni 129 milioni. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Mikel Arteta. Martinelli alifunga mabao 15 msimu uliopita lakini msimu huu bado hajatupia na pia huenda akakosa mechi kadhaa kutokana kuumia kwenye mechi ya ligi dhidi ya Everton wikiendi iliyopita.

1. Erling Haaland - Man City Pauni 215.5 milioni)

Straika huyo wa kimataifa wa Norway alivunja rekodi zote baada ya kufunga mabao 52 katika mechi 53 alizocheza huku Man City ikibeba makombe matatu msimu uliopita. Halaand alianza msimu mpya kwa kishindo akipania kuendeleza rekodi zake na tayari ameshaweka kambani mabao saba kwenye ligi.

Chanzo: Mwanaspoti