Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastraika wa Timu 8 waliobuma Ligi Kuu

Mzize Yanga Konkoni Skudu Mwamnyeto Mastraika wa Timu 8 waliobuma Ligi Kuu

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mastraika wa Yanga, wamefunga mabao mawili tu kwenye Ligi Kuu hadi sasa lakini kazi yao inatimizwa vyema na viungo wao ambao wamepachika mabao 11 jambo ambalo limechangia kuifanya timu hiyo kuwa kinara wa ufungaji katika raundi tano za ligi ikiwa na mabao 15.

Lakini wakati Yanga ikionekana kuwa na uhakika wa mabao licha ya washambuliaji wake kuwa butu, kuna timu nane (8) ambazo ubutu wa washambuliaji wao umegeuka shubiri katika raundi tano ambazo kila moja imecheza hadi sasa kutokana na kufunga idadi ndogo ya mabao, udhaifu ambao umezifanya zisiwe na mwanzo mzuri kwenye ligi.

Coastal Union - Mabao 2

Ikiwa inashika mkia katika msimamo wa ligi, Coastal Union imepachika mabao mawili tu katika mechi tano ilizocheza huku kati ya mabao hayo mawili, moja tu likifungwa na mshambuliaji ambaye ni Hija Ugando.

Namungo - Mabao 2

Kama ilivyo kwa Coastal Union, Namungo FC nayo imefunga mabao mawili tu hadi sasa huku bao moja tu likifungwa na mshambuliaji ambaye ni Fabrice Ngoyo wa Ngoy.

Geita Gold - Mabao 2

Ni miongoni mwa timu zilizofunga mabao mawili katika raundi tano zilizochezwa ingawa yenyewe mabao yake yote yamepachikwa na mshambuliaji mmoja tu ambaye ni Elias Maguli.

Kagera Sugar - Mabao 3

Katika mechi tano zilizopita, Wakata Miwa wa Kagera Sugar wamefunga mabao matatu tu na katika mabao hayo, moja tu ndilo limefungwa na mshambuliaji ambaye ni Gasper Mwaipasi

Singida Big Stars - Mabao 3

Licha ya kusajili kundi kubwa la washambuliaji wenye majina makubwa, hadi sasa timu hiyo ina bao moja tu lililofungwa na mshambuliaji ambaye ni Elvis Rupia huku mawili yakipachikwa na viungo.

Ihefu SC - Mabao 3

Usajili wa Charles Ilanfya na Moubarack Hamza ulitegemewa ungeifanya Ihefu kuwa tishio kwa kufumania nyavu msimu huu lakini hadi sasa washambuliaji hao kila mmoja amepachika bao moja huku timu yao ikifunga mabao matatu tu.

Dodoma Jiji - Mabao 4

Licha ya kufumania nyavu mara nne katika mechi zake tano, Dodoma Jiji ina bao moja tu lililofungwa na mshambuliaji, moja likiwa la kiungo na moja la beki huku lingine likiwa la kujifunga la kipa wa timu pinzani.

Mashujaa- Mabao 4

Ni timu iliyoanza vizuri ligi kwa kuvuna pointi nane katika mechi tano ilizocheza lakini imefumania nyavu mara nne tu ambapo mabao mawili yamefungwa na mshambuliaji Adam Adam huku bao moja likifungwa na beki na lingine kiungo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: