Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa wengi wameomba kuondoka Azam FC - Popat

Popat Azam Nsz Mastaa wengi wameomba kuondoka Azam FC - Popat

Thu, 30 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ amekiri kuwa wachezaji wengi wa kikosi hicho wameomba kuondoka ndani ya klabu hiyo baada ya msimu kumalizika.

Azam wamemaliza katika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya NBC na kufanikiwa kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao, hvyo tayari wameshaanza maandalizi ikiwa ni pamoja na kusajili wachezaji 4 mpaka sasa licha ya kwamba dirisha la usajili bado halijafunguliwa.

“Wachezaji ni wengi wameomba kuondoka, lakini hilo ni suala lililo ndani ya uongozi kwani bado wana mikataba na timu, hivyo mara baada ya msimu kumalizika na kocha kufanya tathmini ya kikosi chake kutakuwa na majibu mazuri nani anaondoka nani anabaki,” amesema Popat.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live