Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa watatu wanaofunga usajili Simba hawa hapa

Peter Simba Data Mastaa watatu wanaofunga usajili Simba hawa hapa

Wed, 27 Jan 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

WAWAKILISHI wa Tanzania katika Ligi ya mabingwa Afrika, Simba watafunga usajili wa Shirikisho la soka Afrika (Caf), kwa kushusha mashine za maana si chini ya wachezaji watatu.

Taarifa kutoka ndani ya Simba, zinaeleza tayari wachezaji hao watatu kati yao wawili wameshafika nchini na muda wowote watatambukishwa na kuanza kazi ya kuitumikia timu hiyo.Mwanaspoti imepata taarifa kuwa nyota hao ni  Mkongomani mmoja, Doxa Gikanjia ambaye tayari amesainishwa mkataba wa miezi sita na sasa yuko katika majukumu ya timu ya taifa ya DR Congo, inayoshiriki mashindano ya Chan, huko nchini Cameroon.

Kiongozi mmoja wa Simba, mwenye maamuzi ndani ya timu hiyo alisema tayari wamemaliza usajili wa Gikanji  na sasa wapo katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa Mzimbabwe mmoja kati ya wawili  ambao tayari majina yao yapo mezani."Wazimbabwe hao ni Peter Muduwa na Talent Chamboko ambao wote wanacheza nafasi ya beki wa kati na tunaweza kumalizana nao wakati wowote kuanzia sasa. ," amesema

Chanzo: mwanaspoti.co.tz