Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa watatu Stars watolewa mchezoni

Wazuiwa Pic Data Stars itashuka dimbani bila ya nyota wake watatu

Sun, 14 Nov 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Wakati kikosi chas Taifa Stars kikivamiwa na wanajeshi wa Madagascar wakia hotelini taarifa mpya ni kwamba wachezaji watatu wamezuiwa kucheza mchezo huo wa baadaye.

Stars itashuka  Uwanja wa Mahamasina jijini Antananarivo nchini Madagascar kuwavaa wenyeji wao katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia Qatar, 2022 huku timu zote zikiwa hazina nafasi ya kwenda kokote.

Mapema asubuhi wanajeshi wa Madagascar walivamia kambi ya Stars na kuzingira vyumba vya baadhi ya wachezaji wakidai kuna baadhi yao wamebainika kuwa na maambukizi ya Uviko 19.

Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Clifford Ndimbo amethibitisha kwamba majibu yaliyokuja kufuatia vipimo vya jana vinadai kuwa mshambuliaji Mbwana Samatta, beki Bakari Mwamnyeto na kipa Aishi Manula wamekutwa na maambukizi.

"Wanadai wachezaji hao ndio wamekutwa na maambukizi kutokana na vipimo hivyo lakini mapema tumefanya vipimo vyetu wenyewe tena zaidi ya mara mbili lakini Samatta,Manula na Bakari wote walikuwa wanaonekana hawana kitu kama hicho,"amesema Ndimbo.

"Bado tunafuatilia taarifa zaidi kwa kuwa hapa tumekuja na msafara wa watu wa serikali na hata wakuu wa TFF na wao wanafanya mawasiliano katika kuondoa hii taharuki lakini mpaka sasa hali ni hiyo kwamba tunaweza kuwakosa wachezaji hawa.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz