Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa wanne Yanga kuikosa Azam FC Fainali ya ASFC Mkwakwani kesho

Mayele, Lomalisa Moloko Mastaa wanne Yanga kuikosa Azam FC Fainali ya ASFC Mkwakwani kesho

Sun, 11 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachezaji wawili wawili wa Yanga, Straika Fiston Kalala Mayele na kiungo Stephane Aziz Ki watakosekana kwenye mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam, utakaopigwa kesho kwenye dimba la Mkwakwani, Tanga.

Sababu kubwa ya wachezaji hao kukosekana kwenye mchezo huo dhidi ya Azam FC, ni kuitwa kwenye majukumu ya timu zao za Taifa.

Mchezo huu wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF , uliopangwa kuchezwa Juni 12, 2023 uko ndani ya Tarehe za FIFA ambazo zinawapa haki Mashirikisho ya mpira wa miguu duniani kuwa na haki ya kumliki mchezaji pindi anapoitwa kwenye timu za Taifa.

Yanga ina wachezaji watano wa nje walioitwa timu za Taifa, Fiston Kalala Mayele, Azizi Ki, Khalid Aucho, Djigui Diarra na Kennedy Musonda.

Taarifa iliyotolewa leo Jumapili Juni 11, 2023 na idara ya habari ya Yanga imeeleza;

"Uongozi wa Yanga umefanya juhudi kubwa za kuwasiliana na Mashirikisho ya mpira wanapotoka wachezaji hao na ulifanikiwa kuwabakisha nyota watatu, Kennedy Musonda, Diarra na Aucho ambao hawa watasafiri nchini mara tu baada ya kumalizika kwa mchezo wa Fainali ya ASFC.

"Lakini kwa Mayele na Azizi Ki, ilishindikana baada ya kuwepo na changamoto ya kupata ndege za kuwasafirisha usiku baada ya mchezo kuwahi kwenye kambi za timu zao za Taifa," imesema taarifa hiyo.

Wachezaji wengine watakaokosekana kwenye mchezo huo wa kesho ni Farid Mussa aliyepata majeraha kwenye mchezo wa Ligi dhidi ya Mbeya City na Jesus Moloko anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: