Hivi karibuni kumekuwa na ushindani kwenye Soka la Afrika hususani kwenye masuala ya uhamisho/usajili, ambapo wachezaji wamekuwa wakisajiliwa kwa fedha kubwa jwenda kwenye vilabu vikubwa hapa Afrika.
Mabingwa wa kihitoria Klabu ya Soka ya Al Ahly inayoshiriki Ligi Kuu nchini Misri ndio inayoongoza kwa kuwalipa wachezaji mishahara mikubwa katika Bara la Afrika.
Wachezaji wawili wanaopokeq mshahara mnono Ahly ni mchezaji wa kimataifa kutoka Afrika Kusini, Percy Muzi Tau na mchezaji wa kimataifa kutoka Tunisia, Ali MaĆ¢loul.
Hawa kila mmoja wamlipwa kiasi cha $100,000 sawa na Tsh 241,456,900.00 kwa mwezi mmoja ambapo kwa mwaka wanavuna zaidi ya Tsh bilioni mbili kila mmoja.