Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa wamshtua Mkude Yanga

Moloko Mkudee Mastaa wamshtua Mkude Yanga

Thu, 26 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo Jonas Mkude ana deni na Yanga na muda wa kuilipa anao, anachotakiwa ni kukaa chini na kutafakari aanzie wapi dhidi ya anaoshindania nao namba ndani ya kikosi hicho, kisha achukue hatua.

Yanga ilimsajili Mkude baada ya kuachwa na Simba ambayo aliitumikia tangu alipopandishwa kutoka kikosi cha vijana 2012 -2023, hata hivyo ameshindwa kupata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo na wakati mwingine amekosekana hata kwenye benchi.

Kabla ya mechi ya juzi ya Yanga dhidi ya Azam FC, katika dakika 450 za michezo mitano iliyopita Mkude alitumika dakika saba tu dhidi ya JKT Tanzania, jambo linaloibua maswali mengi kwa mashabiki kujiuliza kakumbwa na kitu gani.

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi amekuwa akimpa kila mchezaji nafasi ya kucheza, hivyo ni kazi kwao kuonyesha kile kinachotakiwa kwa ajili ya kuisaidia timu lakini kwa Mkude mambo yamekuwa tofauti.

Gamondi aliwahi kusema kwamba;”Kila mchezaji ana nafasi ya kucheza ndani ya kikosi changu, ninachoangalia ni bidii yao mazoezini, kwani lengo ni timu kufanikiwa kwenye malengo yake.”

Hata hivyo, wadau na baadhi ya makocha hawakuwa nyuma kumjenga Mkude kutambua nafasi bora aliyonayo ya kuweka mambo yake sawa kurejesha kiwango chake ili kuendelea kulinda heshima ya jina lake katika soka la Tanzania.

Beki wa zamani wa Simba na Yanga, Amir Maftah alisema bado anaamini Mkude ana uwezo wa kucheza kikosi cha kwanza kwa sharti ya kumuonyesha kocha anachokitaka akifanye.

“Kocha anapompa mchezaji dakika za kucheza anakuwa na maana kubwa ya kuangalia je, anakifanya kile anachotakiwa, ndio maana nasema Mkude ni yeye kujipanga ila bado ana umri wa kucheza na akabadili upepo,”alisema.

Hoja yake iliungwa mkono na staa wa zamani wa Simba na Stars, Steven Mapunda aliyewatolea mifano Clatous Chama na Moses Phiri kwamba mashabiki waliwatetea mbele ya kocha wao Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ilitokana na uwezo wao.

“Ninachokiona kwa Mkude anapaswa kujipanga na kujitoa kweli kweli kurejesha kiwango chake ni kiungo mzuri sana akikaa kwenye mstari. Ukiona mashabiki wamenyamaza na hawamwambii kocha akupange jiulize mara mbili mbili na lazima ukubali ukweli ambao utakubadilisha,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: