Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa waliopigwa chini na Simba wabeba ubingwa

Apr AznNc.jpeg Mastaa waliopigwa chini na Simba wabeba ubingwa

Mon, 22 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Jeshi APR FC ndio Mabingwa wa Ligi Kuu ya Rwanda 2023/2024.

Kikosi cha kocha Thierry Froge kilipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Kiyovu Sports FC jana na kushinda taji la Ligi Kuu mara tano mfululizo.

Ushindi huo umeifanya APR FC kufikisha pointi 63 katika mechi 27 ilizocheza, huku Rayon Sports Fc wakishika nafasi ya pili wakiwa na pointi 51 na Musanze FC pointi 47 katika nafasi ya tatu.

”Tuna furaha sana kwamba baada ya kufanya kazi kwa bidii tumeshinda taji la ligi ,” amesema Kocha wa APR Froge.

APR FC imebeba kombe mwaka wa 1995, 1996, 1999, 2000, 2001, 2003, 2005, 2006, 2007, 2009, 2010, 2011, 2012, 2014, 2015, 2016, 2018, 2020, 2021, 2022, 2023 na mwaka 2024.

Pamoja na nyota wengine, kikosi hicho kina wachezaji waliowahi kupita Simba baadaye wakafungashwa virago kama Sharaf Shibob wa Sudan Kusini, Thadeo Lwanga wa Uganda na aliyekuwa kocha wao wa viungo Zrane raia wa Tunisia ambaye alifariki dunia hivi karibuni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live