Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa walioongoza kutumiwa posti za chuki mtandaoni EPL

Mastaa Chukiiiii Mastaa walioongoza kutumiwa posti za chuki mtandaoni EPL

Tue, 25 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mitandao ya kijamii ina utamu na uchungu wake kwa wanasoka wa Ligi Kuu England.

Kuna wachezaji wamekuwa kwenye wakati mgumu kutokana na kutumiwa sana meseji za lugha chafu kwenye mitandao hiyo, huku mastaa wengine wakiwa na wakati mzuri wa kupata sifa nyingi.

Kwenye Ligi Kuu England, masupastaa Marcus Rashford, Mohamed Salah na Bukayo Saka ndiyo wachezaji waliosakamwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii, huku Manchester United ikiongoza kwa upande wa klabu zilizotumiwa posti nyingi za kusakamwa.

Licha ya kutumiwa meseji hizo za kusakamwa, Saka pia amepokea pongezi nyingi kwenye mitandao ya kijamii, sawa na kinda wa Chelsea, Cole Palmer. Kwa takwimu zilizokusanywa kuanzia Agosti 18, 2023 hadi Mei 19, 2024 hii hapa orodha ya mastaa walioongoza kwa kusakwa kwenye mitandao ya kijamii.

Mastaa walioongoza kutumiwa meseji mbaya

Supastaa wa Man United, Rashford amekuwa mchezaji namba moja kwa kutumiwa mesaji nyingi mbaya kwenye mitandao ya kijamii, ambapo staa huyo wa Old Trafford amekumbana na posti 707,160 za kumtusi kwa msimu wa 2023/24.

Fowadi wa Liverpool, Mo Salah na winga wa Arsenal, Saka wanafuatia kwa kutumiwa meseji nyingi za kusakamwa na mashabiki kwenye mitandao ya kijamii, ambapo mkali wa Anfield, amekumbana na posti za 382,140 za matusi dhidi yake, lakini Rashford akiwaacha kwa mbali wenzake.

Saka, ambaye alikuwa na kiwango bora kabisa kwenye kikosi cha Arsenal kwa msimu uliopita, amemzidi Kai Havertz kwa wachezaji waliotumiwa meseji nyingi za chuki kwenye mitandao ya kijamii, ambapo winga huyo wa England alikumbana na posti 368,300 huku Mjerumani, Havertz alikumbana na posti za hovyo 354,940 za matusi dhidi yake.

Straika wa Manchester City na mtambo wa mabao wa Norway, Erling Haaland, pamoja na ubora wake wa kufunga, hilo halikumfanya akwepe kukumbana na meseji za kusakamwa na mashabiki kutoka kwenye mitandao ya kijamii, alipotumiwa posti 293,800 za kumkashifu kwenye mitandao.

Wachezaji wengine waliokumbana na meseji nyingi za hovyo kwenye mitandao ya kijamii ni Alejandro Garnacho na Harry Maguire, wote wakiwa ni mastaa wa Man United, ambapo wa kwanza alikashifiwa mara 261,380 na wa pili mara 250,000.

Asilimia kubwa meseji walizopokea ni za hovyo

Wakati Rashford akiongoza kwa kupokea meseji nyingi za hovyo kwenye mitandao ya kijamii kwa msimu wa 2023/24, asilimia 27 ilikuwa meseji za chuki dhidi yake, huku mchezaji mwenzake wa Man United, Christian Eriksen, kwenye meseji 75,280 za hovyo alizopokea, asilimia 29 zilikuwa za chuki. Mabeki wa pembeni, Diogo Dalot wa Man United, Oleksandr Zinchenko wa Arsenal na Ben Chilwell wa Chelsea walilingana na Eriksen kwa kutumiwa asilimia 28 ya meseji zao kwenye mitandao ya kijamii kuwa za chuki.

Wakati Cody Gakpo wa Liverpool akilingana na Rashford kwenye asilimia 27, mastaa wawili wa Chelsea, Noni Madueke na Levi Colwill wenyewe wametumiwa asilimia 26 ya meseji za chuki, ambapo wa kwanza alipata meseji za hovyo 96,220 na wa pili meseji 70,540.

Scott McTominay na Maguire, licha ya kucheza vizuri msimu wa 2023/24, nao walisakamwa sana mtandaoni, ambapo McTominay alipokea meseji za chuki asilimia 25 na Maguire asilimia 24.

Timu iliyosakamwa zaidi mtandaoni

Man United inaongoza, huku Arsenal nayo ikiwa kwenye orodha kwa timu za Ligi Kuu England zilizosakamwa sana mtandaoni kwa msimu uliopita.

Man United, ambao ni mabingwa mara 13 wa Ligi Kuu England wamepokea meseji za kusakamwa mara 130,474. Na katika meseji zote walizopokea, asilimia 19 ilikuwa ya chuki dhidi ya timu hiyo.

Arsenal, ambayo imekuwa moto sana chini ya kocha Mikel Arteta inashika namba mbili kwa timu iliyosakamwa sana kwa msimu uliopita kwenye mitandao ya kijamii baada ya kukutana na posti 100,000, wakati Manchester City, Liverpool na Chelsea zinafuatia kwenye nafasi ya tatu, nne na tano mtawalia. Man City imekumbana na posti za kusakamwa mara 55,856, huku Liverpool na Chelsea zenyewe zikisakamwa mara 50,000.

Haaland ndiye mchezaji aliyesakamwa zaidi kwenye kikosi cha Man City, wakati Salah na Cole Palmer wakiwa vinara kwa timu za Liverpool na Chelsea kwa msimu wa 2023/24.

Hata hivyo, wachezaji wa Man United ndiyo walioongoza zaidi kwa kusakamwa kwenye mitandao ya kijamii, ambapo kwenye orodha ya mastaa 50 waliokumbana na meseji nyingi za chuki mtandaoni, miamba hiyo ya Old Trafford ina wachezaji 16.

Wachezaji waliosifiwa sana mtandaoni

Licha ya kuwamo kwenye orodha ya waliochukiwa, Cole Palmer na Kai Havertz wamo pia kwa wachezaji waliopostiwa mara nyingi kwenye meseji tamu za kusifiwa pamoja na kiungo kinda wa Man United, Kobbie Mainoo.

Palmer alikuwa kwenye kiwango bora kabisa huko Chelsea msimu uliopita, alifunga mabao 22 kwenye msimu wake wa kwanza Stamford Bridge, alipata meseji za kusifiwa 521,480. Saka na Haaland walifuatia wakiwa na posti 467,140 na 448,880 mtawalia, licha ya kuwamo pia kwenye orodha ya wachezaji waliotumiwa posti nyingi za chuki.

Mastaa wengine waliosifiwa sana mtandaoni kwa msimu wa 2023/24 ni Havertz, Kobbie Mainoo, Garnacho, Declan Rice na Kevin De Bruyne

Chanzo: Mwanaspoti