Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa waliofunga mwaka kibabe

FEI SAL 2 Mastaa waliofunga mwaka kibabe

Tue, 3 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku tatu tayari zimeshameguka tangu ulipoingia mwaka 2023, lakini bado stori za mwaka 2022 zinaendelea kubamba sehemu mbalimbali.

Kwenye Ligi Kuu Bara kuna nyota ambao wenyewe walimaliza mwaka uliopita kwa kishindo baada ya kufanya vizuri katika klabu zao kwa mwaka huo. Hapa championi Jumatatu linakuletea baadhi yao.

FISTON MAYELE

Kwa sasa ndiye kinara wa upachikaji mabao ndani ya Ligi kuu akiwa na mabao 14. Ukiachana na kufunga mabao hayo kwa mwaka 2022 amebakiza mabao mawili tu ili kuyafikia mabao 16 aliyoyafunga msimu uliopita kwenye ligi hiyo.

Bila shaka Mayele ameufunga mwaka vizuri huku akiwa mfungaji bora jambo ambalo linamfanya staa huyo kujivunia zaidi mwaka huo.

CLATOUS CHAMA

Kwenye suala la kutoa pasi za mabao Chama hana mpinzani kwani ndiye kinara wa asisti akiwa ametoa asisti 11, jambo ambalo linamfanya staa huyo kuufunga mwaka 2022 kwa kishindo kikubwa zaidi.

Chama amekuwa na uwiano mzuri sana wa kutengeneza nafasi za kufunga kwenye ligi kuu huku msimu huu ukionekana kumuendea vizuri kwani asisti 11 alizonazo hakuna ambaye anaonekana atamfikia mapema ndani ya ligi kuu.

SAIDI NTIBAZONKIZA

Kabla ya kutua Simba, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ alikuwa ndiye mfalme ndani ya Geita Gold kutokana na kufunga mabao 4 na kutoa pasi tano za mabao ambapo kwa sasa baada ya kujiunga na Simba amefikisha jumla ya mabao saba na pasi 6 za mabao.

Saido mwaka 2022 ameufunga vyema huku tayari akianza kuimbwa na mashabiki wa Simba kutokana na uwezo wake mkubwa aliouonyesha ndani ya timu hiyo katika mchezo wake wa kwanza tu akifunga mabao 3.

FEISAL SALUM

Feisal Salum mwaka 2022 ulikuwa ni mwaka mzuri kwake ndani ya Yanga, kwani alifanikiwa kufunga mabao 5 na kutoa pasi mbili za mabao.

Licha ya Feisal kuwa na mgororo na Yanga lakini hilo halichangii kwa yeye kushindwa kuhesabika kuwa mmoja kati ya wachezaji ambao wameufunga mwaka kwa kishindo katika ligi msimu huu.

STEPHANE AZIZI KI

Pengine inawezekana asiwe na takwimu kubwa na nyingi ndani ya Yanga au ligi kwa ujumla lakini kiungo huyu mshambuliaji amekuwa gumzo kubwa kwa sasa katika ligi kuu kutokana na mipira ya adhabu anayoipiga kuwa gumzo.

Aziz Ki ameufunga mwaka akiwa na asisti 3 na mabao 4, akiwa mmoja ya wachezaji wa Yanga wenye takwimu za juu.

ABDUL SULEMAN ‘SOPU’

Alianza mwaka 2022 akiwa na majeraha lakini staa huyo ameufunga mwaka vyema kwa kufanikiwa kufunga mabao manne katika michezo yake mwili ya mwisho.

MOSES PHIRI

Pengine asingeumia basi Moses Phiri angekuwa na ameongeza idadi ya mabao katika michezo yake miwili ambayo ameikosa staa huyo wa Simba kutoka Zambia.

Phiri kwa sasa ana jumla ya mabao 10, mabao manne pungufu ya Fiston Mayele, lakini ukweli ni kwamba staa huyo ameufunga mwaka vizuri kutokana kuisaidia Simba kwa kufunga mabao hayo ambayo yalikuwa ni muhimu kweli kweli kwa timu.

Phiri atakosekana katika kipindi cha mwezi mmoja kutokana na majeraha aliyoyapata ya kifundo cha mguu katika mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live