Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa walimlilia Atsu

Christian Atsu 1140x640 Christian Atsu

Mon, 20 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mastaa wa soka wameomboleza kifo cha nyota wa zamani wa Newcastle United, Chelsea na Everton, Christian Atsu baada ya mwili wake kuonekana akiwa amefariki. Atsu alifukiwa na kifusi baada ya tetemeko la ardhi lililotokea Uturuki na maeneo jirani ya Syria tangu Februari 6 mwaka huu.

Atsu alitafutwa na waokoaji tangu tetemeko lenye ukubwa wa 7.8 lilipotokea, awali taarifa ziliripoti nyota huyo wa kimataifa wa Ghana alipatika, hata hivyo taarifa hizo zilikua sio za ukweli baada ya kuthibitishwa.

Taarifa za kupatikana kwa mwili wa Atsu zilitolewa na wakala wa nyota huyo: "Natangaza nikiwa na huzuni kubwa kwamba mwili wa Christian Atsu umepatikana, natuma salamu za rambirambi kwa familia yake na marafiki zake kwa ujumla, nawashukuru wote kwa maombi mliyofanya kipindi chote,"

Baada ya taarifa za kifo cha Atsu, wachezaji wenzake waliowahi kucheza timu ya taifa ya Ghana, akiwemo Andre Ayew waliandika ujumbe mbalimbali kupitia akaunti zao za Twitter na Instagram.

Nayo klabu ya Newcastle iliandika ujumbe wa huzuni kufuatia kifo cha Atsu kwenye akaunti yao ya Instagram: "Christian Atsu ni mchezaji mwenye kipaji cha kucheza soka, tunasikitika amepoteza maisha yake kutokana na tetemeko la ardhi iliyotokea Uturuki.

Chelsea ikaungana na Newcastle kutuma salamu za rambimbi nayo ikaandika ujumbe kupitia akaunti ya Twitter, ujumbe huo ulihusu jinsi gani wameguswa na kifo cha staa huyo aliyewahi kukipiga humo.

Everton ilikua timu ya kwanza kuandika salama za rambimbi kufuatia kifo cha nyota wao zamani aliyewahi kuichezea timu hiyo Atsu.

"Tumesikitika sana na taarifa kuhusu kifo cha Christian Atsu, mwili wake umepatikana kufuatia tetemeko la ardhi iliyotokea Uturuki, kila mtu ameathirika na janga hili ambalo imepoteza maisha ya watu wengi" Taarifa ziliripoti mwili wa Atsu ulipelekwa Ghana kwaajili ya taratibu za mazishi baada ya kupatikana.

Chanzo: Mwanaspoti