Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa hawa walikataa Ofa ya Real Madrid

Pogba With Neymar Mastaa hawa walikataa Ofa ya Real Madrid

Tue, 20 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sio rahisi kwa mchezaji mkubwa kukataa nafasi ya kucheza kwenye timu yenye mafanikio makubwa zaidi barani Ulaya kama Real Madrid. Lakini wapo watakaokataa kwasababu hakuna kinachopendwa na kila mtu.

Hawa hapa wachezaji 5 Bora waliowahi kupiga chini ofa za Real Madrid

1. LUIS SUAREZ

"Wawakilishi wangu waliongea na Real Madrid na kila kitu kilikuwa kinakaribia kukamilika, nilipopokea ofa ya Barca, nikaenda kwasababu ilikuwa ni timu ya ndoto zangu"

2. DAVID VILLA

Mwaka 2008 akiwa Valencia, David Villa alipiga chini ofa ya kujiunga na Real Madrid, miaka miwili baadae akajiunga na Barcelona.

3. NEYMAR

Akiwa na umri wa miaka 13, Neymar alitembelea Bernabeu na kufanyiwa vipimo vya afya ili ajiunge na Real Madrid, wakati huo familia yake haikuwa tayari kuishi mbali na mtoto wao, hivyo wakapiga chini uhamisho huo na miaka kadhaa iliyofuata alikataa ofa yao, akajiunga na Barcelona.

4. SANTI CARZOLA

“Kwenye mpira Kuna mambo mengi sana, ilikuwa ni rahisi kuikataa ofa ya Real Madrid japokuwa ni timu kubwa kwasababu ya kuridhika mahali nilipo na nilikuwa nahisi kuthaminiwa katika klabu yangu ya Villarreal"

"Nilikuwa napenda kuendelea kukua ndani ya Villarreal kwa sababu pia mimi ni mdogo na nimeanza kuitwa timu ya taifa."

5. PAUL POGBA

Mwaka 2016, Pogba aliipiga chini ofa ya Real Madrid na kuamua kurejea Manchester United akitokea Juventus.

"Moyo wangu ulikuwa unaniambia nirudi Manchester, sijui ni kwa nini, Lakini nilifanya hivyo na sijutii chaguo langu, ingawa, labda inawezekana ulikuwa ni uamuzi mbaya"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live