Katika kukikusa upya kikosi cha Wanamsimbazi, za ndani kabisa zinaeleza kuwa mastaa wa Simba Augustine Okra, Nelson Okwa, Ismael Sawadogo na Gadiel Michael ambao tayari wamepewa barua za kwaheri klabuni hapo.
Mastaa hao tayari wamepewa barua za kuachana na timu hiyo baada ya kushindwa kuonyesha uwezo ambao walikuwa wanautarajia kutoka kwao Okrah, Okwa walisajiliwa dirisha kubwa la usajili msimu huu wakati Sawadogo akisajiliwa dirisha dogo huku Gadiel alijiunga na Simba akitokea Yanga msimu wa 2019.
Kati ya mastaa hao waliopewa mkono wa kwaheri, tulifanikiwa kumpata Gadiel Michael ambaye alisema ni kweli mkataba wake unamalizika msimu huu lakini bado hajafahamu hatima yake.
"Ishu ya barua? nakusikia wewe na kuhusu mazungumzo ya mkataba mpya au kwenda timu nyingine bado sijafanya uamuzi wowote hadi sasa nasubiri msimu umalizike, bado kuna michezo miwili mbele natakiwa kucheza na mimi ni mchezaji wa Simba." alisema beki huyo.
Chanzo cha ndani ya Simba kimetueleza; "Tumeondoa wachezaji wawili ambao wanacheza nafasi ya winga na kocha amependekeza kusajiliwa kwa wachezaji wawili kwenye nafasi hiyo mgeni mmoja na mzawa mmoja ambaye anaweza kucheza miguu yote miwili."
Chanzo hicho kimesema kuwa wanaendelea na usajili ili kukiandaa kikosi chao mapema kama mapendekezo ya kocha wao alivyotaka kuona wanasajili mapema ili kuingia kambini mapema kujiandaa na msimu mpya.