Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa hawa Simba, Yanga, Azam ni suala la muda tu

John Bocco Simba Sfsd Mastaa hawa Simba, Yanga, Azam ni suala la muda tu

Sun, 14 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuna timu zinakimbizana kuzipata saini za  mastaa waliotemwa na wanaotajwa kuachwa Simba na Yanga, kabla ya kufungwa kwa usajili wa dirisha Jumatatu Januari 15 saa 5:59 usiku.

Tayari baadhi yao wanatajwa wanaweza wakasaini muda wowote kuanzia sasa na wengine hawajafanya maamuzi wapi wanataka kwenda kufanya

DENIS NKANE - YANGA Winga wa Yanga, Denis Nkane kuna asilimia kubwa anaweza akajiunga na Dodoma Jiji kwa mkopo, imeelezwa kocha Francis Baraza aliyewahi kumfundisha Biashara United ndiye anataka asainiwe.

Kwa upande wa Nkane alipoulizwa juu ya tetesi hizo, alisema "Mimi mwenyewe nasikia ila sijui chochote, ninachofahamu mimi ni mchezaji wa Yanga hadi 2025."

NADO, LYANGA - AZAM Wachezaji wa Azam Iddy Nado na Ayub Lyanga wanatajwa kutafutiwa timu kwa mkopo, kati ya timu zilizotajwa ni Singida Fountain Gate na Namungo.

Msimu uliopita Nado alikuwa na mabao saba, msimu huu ana mabao matatu, wakati Lyanga akiwa na bao moja (2023/24).

JOHN BOCCO - SIMBA Siyo mara ya kwanza jina la nahodha wa Simba, John Bocco kutajwa kuachwa na klabu hiyo, awamu hii pia kuna tetesi za kutaka kulikata jina lake, ambapo timu zinazotajwa kumhitaji ni Ihefu na Singida Fountain Gate.

JESUS MOLOKO - YANGA Jina lake linatajwa kwa kasi ndani ya Yanga kuwa kati ya wachezaji wanaoweza kutemwa na timu inayotajwa anaweza akatolewa kwa mkopo na Singida Big Stars.

JIMYSON MWANUKE-SIMBA Ni kati ya waliondolewa kambini Zanzibar, ambako Simba jana ilicheza fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Mlandege, imeelezwa kama mambo yakienda sawa anaweza akamalizana na Mtibwa Sugar wakati wowote kuanzia sasa.

Ingawa alipotafutwa alijibu "Mimi nipo Zanzibar nasubiri fainali kati ya timu yangu Simba na Mlandege."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live