Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa Yanga watua salama Sauzi kuwavaa Mamelodi

Mudata Mastaa Yanga watua salama Sauzi kuwavaa Mamelodi

Tue, 2 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Young Africans SC imefika salama nchini Afrika Kusini, kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns.

Msafara huo wenye wachezaji 26 na viongozi 12 wa benchi la ufundi wakiongozwa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi, uliondoka Dar es Salaam alfajiri ya leo kwa Ndege ya Shirika la Malawi na kufika Johannesburg nchini Afrika Kusini mchana, kisha kuelekea Jiji la Pretoria ambapo ndipo mchezo huo utapigwa.

Baada ya kutua Afrika Kusini, timu ilipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. James Bwana, sambamba na mashabiki na wanachama wa Young Africans SC wanaoishi Afrika Kusini.

Kwenye msafara huo, wachezaji waliokosekana katika mchezo wa kwanza nyumbani uliomalizika kwa matokeo ya 0-0 wamejumuishwa akiwemo Khalid Aucho, Yao Attohoula na Pacome Zouzoua.

Mchezo huo wa marudiano utachezwa Ijumaa hii ya Aprili 5, kwenye Uwanja wa Loftus Versfeld uliopo Pretoria, Afrika Kusini.

Wachezaji waliosafiri ni; Djigui Diarra, Aboutwalib Mshery, Metacha Mnata, Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Dickson Job, Yao Attohoula, Nickson Kibabage na Lomalisa Mutambala.

Wengine ni; Gift Fred, Zawadi Mauya, Maxi Nzengeli, Pacome Zouzoua, Kennedy Musonda, Mahlatse Makudubela, Jonas Mkude na Farid Mussa.

Pia wapo Clement Mzize, Mudathir Yahya, Khalid Aucho, Augustine Okrah, Joseph Guede, Stephane Aziz Ki, Kibwana Shomari, Denis Nkane na Salum Abubakar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live