Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa Yanga watua Algeria, Gamondi ashusha Presha

Aucho X Aziz KI Mastaa Yanga watua Algeria, Gamondi ashusha Presha

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki amemshusha presha kocha mkuu wa timu hiyo Miguel Gamondi baada ya kutua kambini jana tayari kwa mchezo wao dhidi ya CR Belouizdad Ijumaa.

Mastaa wote wa Yanga ambao walikuwa nje timu zao za taifa wametua nchini Algeria watakuwa na siku moja tu kwaajili ya kujiweka fiti tayari kwa mchezo huo.

Wachezaji hao ni Djigui Diarra, Abuutwalib Mshery, Metacha Mnata, Khalid Aucho, Aziz Ki, Bakari Mwamnyeto, Dikson Job, Mudathir Yahya, Clement Mzize, Ibrahim Abdallah ‘Bacca’ na Nickson Kibabage. Mwanaspoti limepata nafasi ya kuzungumza na Gamondi na Aziz Ki ambao kila mmoja amefunguka mambo mbali mbali kuelekea mchezo huo ikiwa ni pamoja na kuungana wenzake kwaajili ya mchezo wao huo wa kwanza hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Ni wachezaji wengi muhimu walikuwa nje ya timu wakiwa na mashindano muhimu ya kushindania mataifa yao lakini walikuwa na ratiba kuwa ni lazima warudi kuipambania timu kuhakikisha inakuwa na matokeo mazuri nina imani nao,” alisema kocha Gamondi na kuongeza;

“Watafanya vyema hii ni kutokana na kuwa na wachezaji ambao wote wana malengo sawa ishu ya Aziz Ki ilikuwa inazungumzwa sana kutokana na umuhimu wake kikosini lakini naamini katika umoja na uashirikiano wachezaji waliopo Yanga ni bora kila mmoja kwa nafasi yake.”

Gamondi alisema malengo yake yametimia baada ya kuona wachezaji wake wamewasiri kambini wote muda aliokuwa anatarajia ameupongeza uongozi kwa jitihada kubwa walizozifanya.

Kiungo Aziz Ki alilithibitishia gazeti hili kuwa tayari ameungana na kikosi cha Yanga jana na yupo tayari kwaajili ya mapambano.

“Nimeshaanza safari najiunga na wenzangu hii ni kutokana na viongozi walivyofanikiwa kusimamia suala la mimi kuhakikisha naanza safari baada ya kukamilisha kazi yangu kwenye timu yangu ya taifa hilo limefanikiwa na ndio maana nimejiunga na timu ki uharaka zaidi,” alisema Aziz KI aliyefunga mabao mawili kwenye mechi za awali za Ligi ya Mabingwa Afrika na mabao saba ya Ligi Kuu Bara hadi sasa na kuongeza;

“Kuhusu mchezo wenyewe naomba tuzungumze baada ya dakika 90 siwezi kuuzungumzia zaidi sasa naamini utaamuliwa baada ya kuchezwa ila benchi la ufundi limetuandaa kushindana na kupambania pointi tatu muhimu ili kujihakikishia nafasi ya kuendelea hatua inayofuata.” Yanga ambayo imepangwa kundi D na timu za CR Belouizdad, Al Ahly ya Misri na Medeama ya Ghana, itashuka dimbani Novemba 24, mwaka huu ikianzia ugenini katika Uwanja wa 20 August 1955, Algeria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live