Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa Yanga watakaoikosa Namungo leo

Yanga DSM Mastaa Yanga watakaoikosa Namungo leo

Wed, 7 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea Mchezo wa kesho dhidi ya Namungo klabu ya Yanga utakaopigwa leo Jumatano, Desemba 7, 2022 itamkosa winga wao Farid Mussa Malick ambaye alipata maumivu kwenye nyama za paja kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons.

Pia, Yanga watamkosa mshambuliaji wao raia wa Congo DR, Heritier Ebenezer Makambo ambaye bado hajawa fiti baada ya kupata majeraha ya kidole cha mguu.

Wakati huohuo mshambuliaji wa klabu hiyo, Fiston Mayele amerejea kikosini baada ya kukosekana kwenye mchezo uliopita dhidi ya Prisons ambapo alikuwa akiuguza majeraha aliyoyapata kwenye mchezo dhidi ya Ihefu.

Yanga ambao ni vinara wa kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC wakiwa na pointi 35 wanakwenda kucheza na Namungo ambao wapo nafasi ya 9 ya msimamo wa Ligi hiyo wakiwa na alama 18.

Tangu Namungo apande daraja kuingia Ligi Kuu miaka minne iliyopita, amecheza na Yanga na Mara 6 ambapo sare ni 5, Yanga ameshinda mechi moja huku Namungo akiwa hajapata ushindi mbele ya mabingwa hao watetezi.

Unadhani nani ataibuka mshindi leo katika Dimba Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live