Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa Yanga warejea na biti

Bacca Ibrahim Yanga Mastaa Yanga warejea na biti

Thu, 1 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kukosa mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), mastaa wa Yanga waliokuwa Afcon wameanza kurejea na baadhi wataiwahi Kagera Sugar na kutamba kuendeleza ushindi.

Yanga juzi iliibuka na ushindi wa mabao 5-1 mechi ya FA, Jumanne itakuwa ugenini kuwakabili Kagera Sugar wakiwakosa wachezaji wao wawili Stephane Aziz Ki na Djigui Diarra ambao walivuka hatua ya 16 bora ya michuano hiyo na Ki akienguliwa hatua hiyo.

Mastaa ambao tayari wameungana na kambi na kujiweka tayari kwa mchezo huo ni nahodha Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Ibrahim Hamad ‘Bacca’, Mudathir Yahya na Kennedy Musonda.

Job alisema anajua kwa nini hakucheza Fainali za Mataifa Afrika na wala sio ishu, hata kiwango au kimo chake lakini kuna kitu amejifunza kwenye Fainali hizo na sasa anarejea klabuni kwake kuendeleza ubora wake.

Alisema kukaa kwake benchi wala hakujampotezea kitu zaidi ya kumuimarisha na kumkomaza, sasa anarudi Yanga kuendeleza moto wake kwenye mashindano huku akiendelea kujiweka tayari kwa kuitwa tena Taifa Stars.

“Naamini sitakaa benchi kwani na kwenda kujifua vizuri zaidi kama beki. Narudi katika kikosi cha Yanga nikiwa na mzuka mkubwa, ili kujipanga kwa ajili ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu mara tatu mfululizo,” alisema Job.

Nahodha Mwamnyeto alisema wanatambua wana majukumu makubwa ya kufanya mzunguko huu kuhakikisha wanatetea taji wanalolishikilia huku akikiri watakuwa na mwendekezo mzuri kutokana na timu kuongeza nguvu kwenye baadhi ya maeneo.

“Tulipewa mapumziko na ndiyo maana kwenye mchezo wa jana tulikosekana lakini leo ‘jana’ tulitakiwa kuripoti kambini tayari kwa ajili ya mchakamchaka wa kumaliza msimu;

“Natarajia tutakuwa bora na kufanya vizuri ili kutimiza malengo tuliyokuwa tumejipangia mwanzo wa msimu kwa kuhakikisha tunatetea taji hilo linawezekana.” alisema.

Mwamnyeto alisema ongezeko la baadhi ya wachezaji litaongeza chachu ya ufanisi kikosini kwa kuhakikisha kila eneo la timu yao linakuwa bora.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: