Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa Yanga walioachwa Dar wasepa Algeria

Bacca Job Mzize Mastaa Yanga walioachwa Dar wasepa Algeria

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachezaji wa Klabu ya Yanga waliokua wakiitumikia timu ya Taifa, wameondoka nchini jana kuelekea Algeria kuungana na wenzao baada ya mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Morocco kutamatika.

Msafara wa kwanza wa Yanga uliondoka nchini usiku wa kuamkia jana na tayari umeshawasili Algeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria utakaopigwa Novemba 24, 2023.

Akizungumza wakati wa kuondoka, Nahodha msaidizi wa Yanga, Dickson Job amesema; "Tumemaliza majukumu ya Taifa sasa tunelekea kwenye majukumu ya klabu. Tunawaomba mashabiki na Watanzania watuombee, tunaamini tutarejea nyumbani na ushindi."

CR Belouizdad Bingwa wa Ligi Kuu ya Algeria misimu minne mfululizo, 2019/20, 20/21, 21/22 & 22/23. Yanga Bingwa wa Tanzania misimu miwili mfululizo 2021/22 & 2022/23.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live