Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa Yanga ngoma nzito, Musonda, Djuma waanika kila kitu

MUSONDA ER.jpeg Musonda

Fri, 17 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Yanga kimeingia kambini jana kujiandaa na TP Mazembe lakini wachezaji wameweka kikao chao wenyewe na kuchanana ukweli kuhusiana na kilichotokea kwenye mechi ya Monastir na wanachopaswa kufanya sasa.

Djuma Shabaan ambaye ni Mkongoni ameliambia Mwanaspoti kuwa wamekutana kama wachezaji bila makocha wala viongozi wao kisha kukubaliana kwamba wanajipanga sawasawa kuanza kushinda kuanzia mchezo huo utakaopigwa Jumapili Februari 19, pale Uwanja wa Benjamin Mkapa.

"Tumeambiana kabisa kwamba tumewaangusha mashabiki wetu, viongozi na makocha, sisi kama wachezaji hili limetuuma sana, lakini tunarudi,tutaingia vitani na Mazembe,"alisema Djuma ambaye ana nafasi ya kuanza kama beki wa kulia huku akiwafahamu vizuri Mazembe.

"Hatutaingia katika mchezo huu kinyonge hiki ndicho tulikubaliana kama wachezaji katika kikao chetu, tunachowaomba mashabiki waje kwa wingi uwanjani Jumapili.

Mshambuliaji Kennedy Musonda ambaye Kocha wa Mazembe amemtaja kama mtu hatari, alisema Yanga imepoteza ugenini na kwamba kila timu ambazo zimeshinda katika kundi lao walishinda wakiwa kwao na hata timu yao inacheza mbele ya mashabiki wao wakitaka kushinda kuwarudishia heshima.

"Tulipoteza kwa makosa yetu, lakini hatukuzidiwa na Monastir, tumeumizwa na matokeo yale tunarudi kwa nguvu kucheza mchezo wa nyumbani kwani hata hawa walioshinda walitumia faida ya kucheza kwao.

"Makocha wetu waliona makosa yaliyotokea, haiwezi kuwa mechi ileile, tunajua itakuwa ngumu lakini tunataka kushinda mbele ya Mazembe hapa hapa nyumbani,"alisema staa huyo ambaye alisajili kuongeza nguvu kimataifa.

Baada ya Yanga kupoteza dhidi ya Monastir timu hiyo imejikuta ikishika mkia katika kundi lao D linaloongzwa na Mazembe wakifuatiwa na Monastir wakitofautiana faida ya mabao ya kufunga na kufungwa huku  Real Bamako akiwa nafasi ya nne.

KUNDI LA YANGA   P  PTS TP Mazembe       1   3 US Monasir       1   3 Real Bamako      0   0 Yanga            0   0    

RATIBA Yanga vs Mazembe - Feb 19 Bamako vs Yanga - Feb 26 Yanga vs Bamako - Machi 8 Yanga vs US Monasir - Machi 19 Mazembe vs Yanga - Aprili 2.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live