Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa Yanga: Wananchi mmesikika

Yanga Bamako Bns Mastaa Yanga: Wananchi mmesikika

Wed, 1 Mar 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kuambulia sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Real Bamako nchini Mali, mastaa wa Yanga wamewaomba radhi mashabiki lakini wakasisitiza kwamba mechi zijazo ni kufa kupona.

Yanga yenye pointi nne ikishikilia nafasi ya pili kundini nyuma ya US Monastir yenye pointi saba.

Nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto alisema walipambana ndani ya dakika zote tisini makosa madogo waliyoyafanya dakika za mwisho yaliharibu lengo lao la kukusanya pointi tatu lakini hilo halijawavunja moyo kwani wanaamini bado wananafasi ya kufanya vizuri.

"Tuliingia kusaka pointi tatu muhimu lakini dakika 90 zimegawa pointi moja kwa kila timu tunarudi nyumbani kujipanga upya kwa kuhakikisha tunapata matokeo ya ushindi kwenye michezo yote iliyobaki ili kuweza kufikia lengo la kutinga hatua ya robo fainali"

"Haitakuwa rahisi lakini sisi kama wachezaji tumetambua makosa na kikubwa tunakutana na timu ambazo tayari tunafahamu ubora wao na mapungufu yao pia tutakuwa kwenye uwanja wetu wa nyumbani tunawaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuja kutupa sapoti,"alisema staa huyo wa zamani wa Coastal Union.

Mshambuliaji wa timu hiyo, Kennedy Musonda alisema matokeo hayo sio malengo yao kama wachezaji kwa namna walivyopambana na kujiandaa walihitaji kuvuna pointi zote tatu lakini hawajakata tamaa kwa walichokipata kwani kimewaongezea pointi ambazo zitawasaidia baada ya michezo yote.

"Tunajipanga kusawazisha makosa nyumbani ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele timu ina morali nzuri wachezaji wote lengo letu ni moja kutinga hatua inayofuata tutapambana hadi tone la mwisho ili kufikia mnalengo tuliyojipangia,"alisema.

Kipa namba moja wa timu hiyo, Djigui Diarra alisema;

"Hatukutarajia hiki tulichokipata lakini yote kwa yote sisi kama wachezaji tumelipokea hili sasa tumesahau haya matokeo tunajipanga kwa mechi zinazofuata kufikia malengo ya kutinga hatua ya robo fainali kwa kuongoza kundi D hilo linawezekana juhudi na kuamini katika kupambana ni kitu ambacho kitatubeba."

Yanga imebakiza mechi tatu, mbili nyumbani dhidi ya Real Bamako, US Monastir na ile ya TP Mazembe ugenini.

Chanzo: Mwanaspoti