Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa Yanga: Acha Ligi irudi tuwaumbue

Yanga Hanang Mastaa Yanga: Acha Ligi irudi tuwaumbue

Tue, 23 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Acha irudi tu. Mastaa wa Yanga ambao wanaendelea na mazoezi Jijini Dar es Salaam, wametamba kwamba wanatamani warudi uwanjani kukiwasha haswa sasahivi kwani walipojimbia wanafanya kazi kubwa.

Wanaamini kwamba kwa tizi wanaloendelea nalo kuna baadhi ya timu shindani zikikutana nao zitaumbuka uwanjani.

Baadhi ya mastaa wa Yanga ambao wanaendelea kujifua Avic Town, wameliambia Mwanaspoti kuwa wanafurahia maandalizi wanayoyafanya huku wakidai kuwa wanatamani ligi irudi hata kesho kwani wapo fiti kwa ajili ya ushindani.

Mshambuliaji Clement Mzize ambaye wadau wengi walitamani kumuona kwenye Afcon akiwa na Taifa Stars, alisema wanajiweka tayari kwa ajili ya mashindano yaliyo mbele yao na wapo kwenye morali nzuri kwa ajili ya kuendeleza pale walipoishia hasa kimataifa.

“Tupo kwenye morali nzuri na ya ushindani ukizingatia kuna maingizo mapya hivyo tunapambana kuhakikisha tunajiweka kwenye hali ya ushindani ili kuhakikisha kila mmoja anakuwa fiti tayari kwa mapambano,” alisema Mzize ambaye amefunga bao moja msimu huu akitoa asisti tatu.

Kiungo bora wa Uganda, Khalid Aucho alisema wanaendelea vizuri na mazoezi na kila mchezaji anajua nini anafanya kwa ajili ya ligi itakaporudi huku akisisitiza kuwa walipoishia hautakuwa mwanzo na kwamba zaidi watarudi kivingine katika mashindano.

“Yanga inamalengo yake na ndio tunayoyapambania kwa kujiweka tayari kwa kushindana na washindani wetu ili kuweza kufikia malengo bila ya kuhofia ubora wo kutokana na sisi kujiandaa na kuwa imara kwa changamoto zote zitakazokuwa mbele yetu,” alisema Aucho ambaye ni panga pangua kikosi cha kwanza akicheza mechi nane kati ya 11 msimu huu.

Beki Joyce Lomalisa alisema yupo fiti na tayari kwa kuipambania timu yake baada ya kutoka kwenye changamoto ya majeraha amerudi kwenye ushindani akicheza mechi mbili za mashindano ya Mapinduzi.

“Nimerudi nipo imara nimeshapata mechi mbili za mashindano ya Mapinduzi baada ya hapo timu inaendelea na maandalizi na mimi nazidi kuwa imara natarajia kuendelea kuwa imara na tayari kwa ushindani,” alisema Lomalisa ambaye amecheza dakika 495 akikosa mechi tatu kati ya 11 walizocheza.

Lomalisa alikosekana kwenye mechi ya kwanza ya ligi dhidi ya KMC, alikosekana dhidi ya Ihefu FC huku mechi mbili za mwisho kabla ya ligi kusimama (kupisha fainali za Afrika), dhidi ya Mtibwa Sugar na Tabora United hakuwepo baada ya kuumia katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly kwa Mkapa.

Wakati mastaa hao wakisema hayo, Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ameomba mechi za kirafiki ili kuwapima wachezaji wake baada ya mazoezi ya muda mrefu waliyokuwa wanayafanya kambini kwao.

Yanga ipo katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu bara baada ya kucheza mechi 11 za ligi wakishinda kumi na kupoteza mchezo mmoja kwenye mechi hizo wamefunga mabao 25 wakifungwa mabao sita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: