Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa Stars wala kiapo Algeria

TAIFA STARS SHANGWE 1 1140x640 Mastaa Stars wala kiapo Algeria

Thu, 7 Sep 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Nyota wa Taifa Stars, wamejaa upepo huko Algeria ambako watacheza leo, Alhamisi mchezo muhimu dhidi ya wenyeji hao wa kupigania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika 'Afcon' kwa mara ya tatu.

Jeshi la Adel Amrouche lipo tayari huko Algeria kwa mchezo huo ambao Taifa Stars inahitaji ushindi au sare ili kuweka hai matumaini ya kwenda Ivory Coast ambako fainali hizo zitatimua vumbi kuanzia Januari 13 hadi Februari 11, 2024.

Miongoni mwa wachezaji hao ni Simon Msuva ambaye siku chache zilizopita ajiunga na JS Kabylie ya nchini humo, alisema licha ya kuwa ugenini wanaweza kupata matokeo kwenye mchezo huo ambao utachezwa kwenye uwanja wa 19 May 1956, Annaba.

"Fokasi yetu ni kupata ushindi kama itashindikana basi tupate hata sare, wenzetu walishafuzu hatujui wataingia vipi lakini jambo muhimu kwetu ni kwamba tumekuwa na maandalizi mazuri ambayo naamini yatatusaidia kufanikisha kile ambacho ni shabaha yetu," alisema Msuva anayeongoza kwa mabao kwa timu ya Stars kwenye Kundi F akiwa amefunga mawili.

Kwa upande wa beki wa kati, Dickson Job alisema kwa maandalizi mazuri yaliyofanyika Tunisia yanawapa nguvu ya kuona matokeo mazuri katika mchezo wa leo.

Aidha alisema jambo kubwa lililopo kwa wachezaji sasa ni kuangalia mchezo huu kama fainali.

“Tunakwenda kucheza kama fainali na sio kufuzu tu kwani hitaji letu ni kuiwakilisha nchi vyema hivyo tutatoka na ushindi. Afcon ni yetu na tunataka kuwaonyesha Watanzania kwa ujumla kuwa tumekuja kupambana kwaajili ya heshima ya Taifa na timu kwa ujumla,” alisema Dickson.

Katika mechi ya kwanza baina ya timu hizo uliochezwa Dar es Salaam, Stars ilipoteza kwa mabao 2-0, lakini rekodi inaonyesha Stars haijawahi kuifunga Algeria zilipokutana kwenye mechi za mashindano au kirafiki na mara ya mwisho kuvaana nchini katika mechi ya marudiano ya kuwania fainali za Kombe la Dunia za 2018 Tanzania ilikandikwa mabao 7-0 baada ya sare ya 2-2 nyumbani.

Chanzo: Mwanaspoti