Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa Simba waondoka timu za Taifa

Simba Kikosi 2 Mastaa Simba waondoka timu za Taifa

Sun, 27 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachezaji wa Klabu ya Simba SC waliokuwa Kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania wamepewa ruksa ya kuondoka kambini hapo na kurejea Klabuni Simba SC na hii leo wataingia kambini pamoja na wenzao ambao hawakuitwa Kwenye Timu zao za Taifa.

Uongozi wa Simba SC uliwaombea ruhusa Wachezaji wao wote walioitwa Kwenye Timu zao za Taifa ambao Ni Peter Banda,Aishi Manula,Mohamed Hussein,Shomary Kapombe,Kibu Denis,Mzamiru Yassin na Jonas Mkude kwaajili ya kupata mda zaidi wa kujiandaa na Mchezo wa mwisho wa Kombe la Shirikisho hatua ya Makundi dhidi ya US Gendermarie.

Mchezo huo utachezwa Jumapili ya April 3,2022 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kuanzia saa moja kamili usiku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live