Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa Simba wala kiapo kuiua Al Ahly

Simba Safari Misri Mastaa Simba wala kiapo kuiua Al Ahly

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba imewasili jijini Cairo nchini Misri tayari kwa mchezo wa kesho wa marudiano ya African Football League dhidi ya Al Ahly lakini mastaa Simba wapania kuitoa wapinzani wao kwao.

Simba inahitaji ushindi au sare yoyote ya mabao kuanzia 3-3 kusaka nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na mabingwa hao wa Afrika katika mchezo wa kwanza.

Mfungaji wa bao la kwanza la Simba kwenye mechi ya mkondo wa kwanza iliyopigwa kwa Mkapa Ijumaa iliyopita, Kibu Denis amesema “Ahly ni timu kubwa lakini hata sisi ni wakubwa, kila kitu kinawezekana kwenye soka. Tuna timu nzuri na kila mchezaji anajituma huku tukiwa na ushirikiano wa kutosha.”

“Zitakuwa ni dakika 90 za nguvu, tutapambana hadi mwisho na lengo ni kutinga nusu fainali.”

Wakati Kibu akiyasema hayo naye beki wake wa kulia Shomari Kapombe amesisitiza akisema wanahitajika kuipa presha safu ya ulinzi ya waarabu hao ambayo inafanya makosa.

"Mabao mawili ambayo wameyaruhusu kwenye mchezo mmoja dhidi ya yetu ndio mabao ambayo waliyaruhusu ndani ya mechi zao tisa zilizopita hapa maana yake tunatakiwa kuwa sawa kwenye usham-buliaji kwa kuwa safu yao ya ulinzi inafanya makosa,"amesema Kapombe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live