Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa Simba waifunika Yanga

79966 Insta+pic

Tue, 15 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

OKTOBA 2010, wataalamu wa masuala ya kompyuta, Kevin Systrom na Mike Krieger waligundua mtandao wa Instagram ambao umekuja kurahisisha namna ya utoaji wa habari na kuwaweka watu karibu kupitia mtandao huo unaokutanisha kwa urahisi watu wa aina mbalimbali.

Baada ya wawili hao kugundua mtandao huo walikubaliana na Facebook ili kuuendeleza na kufanyia marekebisho sehemu ambazo zilikuwa na upungufu na kuanzia hapo mitandao hiyo imekuwa sehemu ya kampuni moja inayofanya kazi kwa ushirikiano na Mark Zuckerburg aliyegundua Facebook.

Mwaka huohuo, walijaribu jinsi mtandao huo unavyofanya kazi ambapo walianza kutumia mfumo wa IOS ili kuona kama unaweza kufanya kazi kama walivyotarajia, walifanikiwa kwenye hilo na kwa mara ya kwanza Instagram ilianza kufanya kazi kupitia mfumo wa IOS. IOS ni mfumo wa ufanyaji kazi wa simu ulioanzishwa na kuendelezwa na kampuni ya Apple.

Mwaka 2012 walianzisha mfumo mwingine wa Adroid ambao ulikuja kurahisisha upatikanaji wake kwa kila mwenye smartphone, tofauti na mara ya kwanza ilivyokuwa kwa wenye simu za Apple tu.

Instagram ni nini

Ni mtandao shirikishi unaoruhusu mtu kutuma au kuchapisha picha na video na watu kutoa maoni yao kuhusu machapisho hayo.

Pia Soma

Advertisement
Kwa mujibu wa mtandao wa SAG Ip unaohusiana na masuala ya teknolojia wa nchini Marekani, Instagram inashika namba nne kwa kupakuliwa duniani, na mpaka sasa umepakuliwa mara bilioni tano, WhatsApp ikishika namba moja.Mtandao huo unatumiwa na watu mbalimbali nchini Tanzania na duniani na umekuja kurahisisha baadhi ya mambo ikiwemo utoaji habari na kuwaweka watu karibu zaidi wakiwemo maarufu na mashabiki wao.

Nchini Tanzania, Instagram inatumiwa na watu wengi wakiwamo wachezaji, wasanii, viongozi na wengine maarufu na wasiokuwa. Pengine kuna ushindani ambao watu wengi wamekuwa wakijuvunia kuwa nani mwenye wafuasi wengi zaidi kuliko mwingine kwenye mtandao huo.

 Gazeti hili linakuleta wachezaji 10 kutoka Ligi Kuu Bara ambao wanaongoza kwa kuwa na wafuasi wengi kwenye mtandao wa Instagram.

Mohammed Hussein

Huyu ndiye ‘mkubwa wao’ anayeongoza kwa kuwa na wafuasi wengi kwenye mtandao huo akiwa na wafuasi zaidi ya 370,000. Beki huyo wa Simba mpaka sasa ameweka zaidi ya machapisho 370. Kwa jinsi mchezaji huyo anavyopenda mtandao wa Instagram haipiti wiki bila kuweka chapisho lolote binafsi au akiwa na wachezaji wenzake.Nahodha huyo msaidizi wa Simba huwa anafurahia mitandao kwa kujumuika na wachezaji wenzake kama Jonas Mkude na Said Ndemla.

Aishi Manula

Kipa huyo wa zamani wa Azam anashika nafasi ya pili kwa kuwa na wafuasi wengi akiwa na wafuasi zaidi ya 270,000 huku akaunti yake ikiwa na tiki ya blue kwa maana inatambulika na wenye mtandao huo. Aishi ni kama Ndemla huwa mvivu sana wa kutupia picha kwenye ukurasa wake na wakati mwingine anaweza kukaa kimya hata wiki moja bila kuweka chochote kwenye ukurasa wake.

 

Jonas Mkude

Pengine Jonas Mkude ndiye mvivu wa mitandao kuliko wachezaji wote watajwa katika makala hii, licha ya kushika nafasi ya nne kwa kuwa na wafuasi 208,000 lakini hana chapisho 1o1ote tu.

Mpaka kufikia Oktoba 9, Mkude alikuwa hajaweka chapisho lolote tangu Septemba 19 mwaka huu alipoweka picha akiwa na Erasto Nyoni mazoezini.

 

Said Ndemla

Kwa kawaida Ndemla huwa mvivu wa kuchapisha kitu chochote kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na wafuasi zaidi ya 230,000 hivyo kushika nafasi ya tatu kwa wachezaji wa ndani kwa kuwa na wafuasi wengi.

Ndemla anaonekana hana mapenzi sana na mitandao ya kijamii kwani pamoja na kuwa na wafuasi wengi idadi ya machapisho yake ni ndogo zaidi ya 140 tofauti na wachezaji wengine.

 Juma Kaseja

Kama huu mtandao ungekuwa umeanzishwa miaka ya 15 iliyopita, basi mkongwe huyu pengine angekuwa mwenye wafuasi wengi zaidi kuliko mchezaji yeyote nchini.

Hilo linatokana na kuwa kwenye soka kwa muda mrefu pamoja na kuwa kipenzi cha mashabiki wengi nchini kutoka katika timu tofauti kama Simba, Yanga KMC na Taifa Stars.

Kaseja anashika nafasi ya tano akiwa na idadi ya wafuasi zaidi ya 190,000. Kwa Kaseja mitandao ni sehemu ya kufurahi mara nyingine huchapisha video akiwa anacheza muziki na hata mazoezini.

 

Meddie Kagere

Mtambo huo wa mabao kutoka Rwanda unashika nafasi ya sita kwa kuwa na idadi kubwa ya wafuasi Instagram akiwa na zaidi ya watu 180,000. Idadi kubwa ya wafuasi wa mchezaji huyo iliongezeka kwa kasi baada ya kuanza kuitumikia Simba mwaka mmoja uliopita akitokea Gor Mahia ya Kenya.

Wengi wanamfuata mchezaji huyo kutokana na ushawishi wa kufunga mabao kitu kinachompa faida ya kuongeza wafuasi kila kukicha.

 

Juma abdul

Beki huyo wa kushoto wa Yanga anashika nafasi ya saba kwa wachezaji wenye mashabiki wengi katika mtandao huo na tayari amekusanya ‘kijiji cha watu’ zaidi ya watu 179,000 kwenye mtandao wa Instagram.

Mara nyingi mchezaji huyo anatumia mtandao huo kuchapisha picha akiwa na wachezaji wanzake au mazoezini, na mara nyingine akiwa na familia yake.Kubwa zadi anapenda kumuweka mtoto wake wa kike anayeitwa Carishma Juma.

 

Deus Kaseke

Kiungo huyo kutoka Jangwani hajapishana hata kidogo na mchezaji mwenzake wa Yanga Juma Abdul, akiwa na idadi ya watu 179,000.

Ni mara chache kumuona amechapisha picha katika mazingira ya myumbani kwake au mtaani, picha nyingi anazoweka ni zile akiwa mazoezini au uwanjani.

Ukiingia kwenye ukurasa wake wake wa Instagram umesheheni rangi za njano na kijani tu, maana yake ni kuwa mara nyingi anaonekana kwenye jezi za Yanga.

 

Ramadhan Kabwili

Kipa wa zamani wa timu ya vijana ya Serengeti Boys kwa muda mfupi ameweza kupenya na kuwapita baadhi ya wakongwe akiwa na zaidi ya wafuasi 170,000. Uwezo na ushawishi wa mchezaji huyo hasa akiwa bado mdogo ni sababu kubwa iliyomfanya mpaka sasa kuwa na idadi kubwa kiasi hicho na iliongezeka baada ya kulamba dili na Yanga.

Kabwili akiwa na idadi hiyo yupo nyuma ya kiungo mshambualiaji Ibrahim Ajib wa Simba.

 

Ibrahim Ajib

Ni idadi ndogo sana amepishana na kipa Ramadhan Kabwili, Kaseke, Juma Abdul na Kagere ambapo Ajib ana wafuasi 183,000.

Mara nyingi Ajib anatumia Instagram kwa ajili ya kufurahi na wachezaji wenzake anapokuwa mazoezini na hata mitaani kwao kipindi cha mapumziko. Anapenda kuonekana kwenye picha na wachezaji Said Ndemla na  Mohammed Hussien na wakati mwingine familia yake.

 

HITIMISHO 

Kwa ujumla wachezaji kutoka klabu ya Simba wanaonekana kuwa ni wengi kuliko kutoka Yanga ambao wanaongoza kwa kuwa na wafuasi wengi kwenye mtandao huo. Katika wachezaji 10 waliotajwa Simba imeipiga Yanga bao kwa kutoa wachezaji sita, Yanga ikitoa watatu.

Chanzo: mwananchi.co.tz