Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa Simba wafunguka kinachoendelea ndani ya klabu

Simba Final Train.jpeg Wachezaji wa sasa wa Simba

Thu, 11 Apr 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Manguli wa zamani wa Simba, hawaridhiki na hali ya mambo ndani ya klabu hiyo. Wameliambia Mwanaspoti jana baada ya kula ubwabwa wa Eid kwamba kuna ulazima wa viongozi wao (pichani) kujitokeza hadharani kuzungumza na wachezaji na wanachama wao.

Wanadai kwamba kitendo cha Simba kuondolewa kwenye mashindano mawili ndani ya muda mfupi siyo jambo la kawaida na hata kisaikolojia kila mmoja atakuwa amevurugwa.

Simba iliondoshwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robofainali na Al Ahly sikuchache zilizopita kabla ya kutua Kigoma walipotolewa tena kwenye Shirikisho na timu changa ya

Kocha na mchezaji wa zamani wa Simba, Abdallah Kibadeni alisena ni muda wa viongozi kutoka na kuzungumza ili kuwarudisha wachezaji kwenye morali na kuweka mambo sawa kwani mshtuko uliotokea ni mkubwa na unahitaji utulivu akili kabla ya kufanya uamuzi mpya.

"Sio hali ya kaiwaida timu inapoteza kuanzia Ligi ya Mabingwa Afrika sasa wamepoteza taji la FA viongozi wapo kimya inaleta picha mbaya kwani hata wachezaji wanajiona wapo kwenye hali ya kawaida kufungwa," alisema staa huyo anayeshimika kwa hattrick za kwenye dabi.

"Simba ni timu kubwa na timu shindani hivyo matokeo mabaya wanayoyapata licha ya ushindani uliopo lakini kuna namna viongozi wanapaswa kutoka na kutoa kauli ili kurudisha Simba kwenye hali nzuri itakayorudisha morali na ushindani," alisema.

Nyota wa zamani wa Simba, Bmmanuel Gabriel 'Batgoal' amewataka viongozi wa Simba kukaa na wachezaji wao kutambua shida ni nini baada ya kuona timu hiyo imekosa mchezaji ambaye anakufa nayo. Gabriel amefunguka hayo siku moja baada ya Simba kutolewa hatua ya 16 bora Kombe la FA kwa penati 6-5 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Alisema haoni upambanaji wa wachezaji kila mmoja anafanya kile anachoona sawa tofauti na misimu mitatu nyuma timu hiyo ikitamba kwa kutwaa mataji na mastaa wakionyesha soka la kuvutia.

"Viongozi wana kila sababu ya kukaa na wachezaji wajue shida iko wapi kabla ya kujikuta wanapoteza kila kitu msimu huu kwani nafasi ya ubingwa bado ipo kama timu itatulizwa na kupewa majukumu kwa wachezaji kuhakikisha wanachezakwa kuipambania,"alisema na kuongeza;

"Unajua viongozi pia wanaweza kuwa sababu kwa kuwaacha wachezaji wafanye wanachojisikia pia kuna wachezaji tayari wanajikuta wao ni wakubwa ndani ya klabu kutokana na namna viongozi wanavyowalea hii sio sahihi mazungumzo yafanyike haraka,"alisema staa huyo aliyekuwa akisifika kwa kutupia dhidi ya Yanga sambamba na staili zake za kutengeneza nywele.

Simba imecheza mechi 19, imeshinda 14, sare tatu na imefungwa michezo miwili, ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu, inamiliki pointi 45, ikizidiwa pointi mbili na Azam (47) na ipo nyuma ya pointi saba dhidi ya Yanga, ikitokea wapinzani wake wakapoteza baadhi ya michezo na ikashinda mechi yote iliyosalia inaweza kunyakua ubingwa.

Idadi ya mabao inayomilikiws na Simba ni 38 ya kufungwa ni 18, wakati Yanga inamiliki mabao 49 imefungwa mabao 11, Azam ina mabao ya kufunga 47 na ya kufungwa 16, hivyo licha ya kuwa nyuma kwa mchezo mmoja, washambuliaji wakitulia wanaweza wakafunga mabao mengi ya kuwafikia wapinzani na kuzidi.

Kwenye msimamo wa wafungaji wanaoongoza kwa mabao 13 ni Aziz Ki (Yanga), Feisal Salum 'Fei Toto (Azam), Wazir Jonior wa KMC ana mabao 11, huku anayeongoza Simba haijafikisha mabao 10, hilo si kikwazo cha kunyosha mikono juu.

Kiungo wa Simba Said Ntibanzokiza 'Saido' ana mabao saba, akifuatia Clatous Chama mabao sita, huku wakiwa bado hawajavunja idadi ya mabao manane yaliyofungwa na Jean Baleke aliyeondoka.

Mataji iliyokosa Simba msimu huu hadi sasa ni Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, kombe la Mapinduzi na michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC). Hesabu zilizobaki kwa Simba ni kuchukua Ligi Kuu Bara ingawa nako haina uhakika zaidi kwani hadi sasa inashika nafasi ya tatu na pointi 45 nyuma ya Azam FC iliyopo

Chanzo: Mwanaspoti