WACHEZAJI wa klabu ya Simba wameonyesha kuwa na morali ya hali ya juu katika mazoezi yao leo asubuhi yaliyofanyika katika uwanja wa Mkapa.
Simba leo imefanya mazoezi yao ya mwisho wakijiandaa na mchezo wao wa kesho dhidi ya Raja Casablanca katika kundi C Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mwanaspoti ambalo lilishuhudia mazoezi hayo, mastaa wa Simba walikuwa na morali kabla ya mazoezi kwani sura zao zilionyesha kuwa na furaha.
Wachezaji wote walifika uwanjani saa 3:30 asubuhi wakiwa wamevaa sare na moja kwa moja walienda uwanjani na wenyewe walijipanga kwenye makundi na kuanza kucheza changamsha mwili.
Ilipofika saa 3:45 kocha mkuu wa timu hiyo, Roberto Olivier ‘Robertinho ‘ aliingia uwanjani na wasaidizi wake kisha na kuanza kuangalia uwanja.
Saa 3:56 Robertinho alianza kutoa program na wachezaji wake waliifata vilivyo kwa kila hatua.
Robertinho aliwataka wachezaji wake kwanza waichangamshe zaidi mwili kwa mazoezi ya viungo kama kukimbia kwenye koni kwa spidi.
Zoezi lingine alilowapa ni wachezaji wenyewe kupimana misuli kwa kuvutana kwa kushikana kisha wanaachiana na kukimbia kwa spidi.
Mazoezi hayo yalionyesha mastaa wote wa Simba kufanya vizuri hadi dakika 15 za awali zilipomalizika.
Wachezaji waliokuwepo kwenye mazoezi hayo ni Aishi Manula, Beno Kakolanya, Ally Salim, Beno Kakolanya, Shomari Kapombe, Israel Patrick, Mohamed Hussein na Gadiel Michael.
Henock Inonga, Kennedy Juma, Joash Onyango, Nassor Kapama, Pape Ousmane Sakho na Moses Phiri.
Wengine ni John Bocco, Saido Ntibazonkiza, Jonas Mkude, Sawadogo, Mohamed, Kibu Denis, Jimmyson Mwanuke na Jean Baleke.