Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa Simba, Yanga walioitwa Taifa Stars kurejea nchini

Mzize Manula Mastaa Simba, Yanga walioitwa Taifa Stars kurejea nchini mapema

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekubaliana na vilabu vya Simba na Yanga kuwa wachezaji wa vilabu hivyo waliopo timu ya Taifa iliyopo Azerbaijan kwa ajili ya michezo ya FIFA Series 2024 wataaanza safari ya kurejea nchini Machi 23, mara baada ya mchezo wa kwanza dhidi ya Bulgaria Machi 22.

Kwa mantiki hiyo, mastaa hao watacheza mchezo mmoja tu na kurejea nyumbani kujiunga na vikosi vya vilabu vyao huku mchezo wa pili wakiwaachia wenzao ambao hawana mechi za CAFCL.

Makubaliano hayo yamefikiwa ili kuwapa muda wachezaji wa Simba na Yanga kujiandaa na michezo ya mkondo wa kwanza ya robo fainali ya klabu bingwa Afrika (CAF Champion League).

Simba watacheza na Al Ahly, Machi 29 huku Yanga watacheza na Mamelodi Sundowns Machi 30 michezo yote itachezwa saa 3:00 usiku kwenye Dimba la Benjamin Mkapa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live