Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa Simba, Yanga kazi wanayo

Kumekucha Mapinduzi Cup! Simba, Yanga Ndani! Mastaa Simba, Yanga kazi wanayo

Tue, 2 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuna mastaa Simba na Yanga waliocheza dakika chache, wamekalia kuti kavu kuendelea kusalia ndani ya vikosi hivyo na makocha wanaboresha baadhi ya maeneo kupitia dirisha dogo lililo wazi kwa sasa.

Tayari Yanga imesajili Shekhan Ibrahim Khamis kutoka JKU ya Zanzibar ambaye ni kiraka anayeweza kucheza namba 6, 8 na wingi za kulia na kushoto.

Kwenye namba hizo kuna mastaa ambao hawapati nafasi mara kwa mara kama Jesus Moloko (winga), Salum Abubak ‘Sure Boy’ (8) na Jonas Mkude (6), pia imemsainisha mkataba wa miaka miwili winga wa zamani wa Simba, Augustine Okrah.

Ndani ya kikosi cha Yanga, kuna mastaa wanaotajwa kuombwa kwa mkopo kutokana na nafasi zao kuwa finyu kama Crispin Ngushi ambaye kwenye Ligi Kuu amecheza dakika 11 tu dhidi ya Mtibwa Sugar, ambaye anatakiwa kwa mkopo na JKT Tanzania na Mtibwa.

Wachezaji wengine waliocheza dakika chache ni Gift Fred dhidi ya Geita Gold (dakika tano), Mtibwa (dakika 16), Jonas Mkude dakika saba, dhidi ya JKT Tanzania na saba dhidi ya timu yake ya zamani, Simba.

Kwa upande wa Simba waliocheza dakika chache ni Shaaban Chilunda dakika moja dhidi ya Prisons, dk16 (vs Ihefu) na  dk31 (vs Namungo), Abdallah Hamis dakika tano dhidi ya KMC, Nassoro Kapama (0), Aubin Kramo (0), Hussein Kazi dakika tano dhidi ya KMC, David Kameta (0), Jimson Mwanuke (0), Israel Mwenda dhidi ya Dodoma Jiji dakika 10, Coastal Union dakika 15, Singida Big Stars dakika nne na Ihefu moja, Hussein Abel (0) na Ahmed Feruz (0), hizo ni data za Ligi Kuu.

Inasemekana Abel kaombwa kwa mkopo na Mtibwa na Mashujaa, na hao wengine viongozi wanawatafutia timu za kuwapeleka kwa mkopo ili wakaboreshe viwango vyao.

Kutokana na data za wachezaji hao, beki wa zamani wa Simba na Yanga, Amir Maftah alisema kuvaa uzi wa klabu hizo ni fursa kubwa kwa mchezaji kutengeneza maisha yake,  kinachotakiwa ni bidii na kuonyesha kiwango cha kuisaidia timu.

“Kusajiliwa ni kitu kimoja na kucheza ni kitu kingine, mchezaji akipata fursa hiyo lazima ajitume kwa bidii na kuhakikisha kiwango chake kinakuwa msaada kwa timu yake,” alisema.

Hoja yake ilikwenda sambamba na ya beki wa zamani wa Simba, Mohamed Banka aliyesema “Ukipata nafasi ya kucheza klabu kongwe unawajibika kujituma kwani ni timu zenye malengo ya ubingwa hivyo mchezaji analazimika kuonyesha anastahili kuwepo ndani ya timu hizo.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live