Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa Prisons kuwania mjengo

Kimenya Mjengo Mastaa Prisons kuwania mjengo

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wachezaji, Salum Kimenya, Jumanne Elfadhili, Yona Amos na Zabona Hamis wameanza mtifuano katika vita ya kuwania tuzo ya mchezaji bora ndani ya kikosi hicho msimu atakayeondoka na zawadi ya nyumba ya kisasa kutoka kwa mdhamini wao mkuu.

Prisons iliingia mkataba wa mwaka mmoja na Kampuni ya Bens Agro Agro Star wenye thamani ya Sh150 milioni na pamoja na mambo mengine ila mdhamini huyo aliahidi pia kutoa nyumba ya kisasa kwa mchezaji bora wa kikosi hicho msimu huu.

Mchezaji huyo atapatikana kupitia kwa mashabiki ambao watapiga kura kumpata mshindi na hadi sasa wanne ndio wanaopewa zaidi nafasi.

Kipa, Amos ndiye aliyecheza michezo mingi akiwa amecheza 16 akiwa na 'Clean Sheets' sita na kuiweka timu hiyo nafasi ya saba na pointi 20.

Kwa upande wa Elfadhili ambaye ni nahodha amecheza michezo 15 na kati ya hiyo amefunga mabao matatu na kuchangia pia matatu 'Assisti' huku kwa Zabona aliyekuwa kwenye kiwango bora hadi sasa akifunga matatu na kuchangia mawili.

Shabiki wa timu hiyo, Beny Igwe alisema baada ya Balua kuondoka, kwa sasa vita ipo kwa nyota hao huku mchujo ukiendelea kutokana na mchango wa kila mmoja.

"Haina maana wengine hawafanyi vizuri au tayari tumepata mshindi ila kazi hii itakuwa hadi mwisho wa msimu japo kwa sasa hao ndio wanaoongoza kwenye orodha," alisema Igwe.

Chanzo: Mwanaspoti