Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa Ihefu wakuna kichwa, Maxime awatuliza

Ihefu Kimataifaaaa Mastaa Ihefu wakuna kichwa, Maxime awatuliza

Tue, 2 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Nahodha wa Ihefu, Joseph Mahundi amesema licha ya kiwango bora walichonacho wachezaji, lakini ishu ya kukosa matokeo mazuri inawaumiza kichwa sana akiahidi Ligi Kuu ikirejea watabadilika.

Ihefu haijawa na mwenendo mzuri kwenye Ligi Kuu ikiwa nafasi ya 13 kwa pointi 13 na inatarajia kurejea uwanjani Februali 18 kuwafuata Kagera Sugar katika mwendelezo wa michuano hiyo.

Timu hiyo itakuwa chini ya kocha mpya, Mecky Maxime aliyetangazwa hivi karibuni akiziba nafasi ya Zuberi Katwila aliyetimkia Mtibwa Sugar kuhakikisha Ihefu inafanya vizuri.

Mahundi aliliambia Mwanaspoti kuwa wachezaji wamekuwa na kiwango bora wakiipambania timu, lakini matokeo yamekuwa si ya kuridhisha akiahidi baada ya mapumziko watarejea kwa nguvu mpya.

Alisema kipindi cha mapumziko ni muda wa kujisahihisha akiwaomba wenzake kuendelea kufanya mazoezi yao binafsi ili wanaporejea kambini waendeleze ubora na kubadili upepo.

“Sisi tunaona kiwango kipo juu na kila mmoja anatimiza wajibu wake kimsingi ni kutumia muda huu wa mapumziko kufanya mazoezi binafsi ili kurejea kwa utofauti na kuipambania zaidi timu,” alisema nahodha huyo.

Kwa upande wa kocha mkuu wa timu hiyo, Maxime alisema Ihefu haina mapungufu mengi hivyo atakapoanza kibarua rasmi atasahihisha makosa na kuiweka pazuri katika msimamo.

“Bado sijaanza kazi nipewe muda nifike nikutane na wachezaji wenyewe ambao ndio wanaocheza, mimi kazi yangu kufundisha ila kwa ujumla naamini tutafanya vizuri,” alisema kocha huyo.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: