Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa Geita wamwagiwa noti kuimaliza Yanga Azam Complex

Geita Gold FC Mpunga Mastaa Geita wamwagiwa noti kuimaliza Yanga Azam Complex

Sat, 11 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati kikosi cha Geita Gold kikifanya maandalizi ya kuivaa Yanga keshokutwa katika Uwanja wa Azam Complex, mabosi wa timu hiyo wameongoza motisha wakisema watanunua ushindi utakaopatikana dhidi ya vinara hao wa Ligi Kuu Bara.

Geita Gold ambayo inakamata nafasi ya tano na pointi 34 itaivaa Yanga ya moto ambayo imetoka kufanya vizuri kwenye Kombe la Shirikisho Afrika huku wenyeji wakiwa na rekodi nzuri ya kushinda michezo yote minne waliyokutana.

Mwenyekiti wa bodi ya klabu ya Geita Gold, Zahra Michuzi alilitonya kuwa kila bao litanunuliwa katika mchezo huo huku akigoma kutaja thamani watakayoweka kwa mabao hayo.

“Ujumbe wangu kwa wachezaji kuelekea mchezo huu ni kwamba nawatakia kila la kheri na ushindi wowote tutaununua, naomba ibaki hivyo (akigoma kutaja bei),” alisema Zahra ambaye pia ni Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Geita.

Naye, Kocha msaidizi wa timu hiyo, Mathias Wandiba alisema vijana wake wako tayari kwa mchezo huo baada ya kufanya maandalizi mazuri huku akitamba kuwa rekodi ya kinyonge mbele ya Yanga haiwaogopeshi kwani wakati huu wamejipanga kuambulia chochote.

“Mechi za nyuma hatujafanya vizuri dhidi ya Yanga lakini huu ni mchezo mwingine kwa hiyo tageti yetu ni kupata matokeo mazuri inawezana kabisa kama vijana wakitimiza uwajibika uwanjani na kufuata maelekezo tunayoendelea kupeana mazoezini,” alisema Wandiba.

Akizungumzia mwendelezo wa ubora wa wachezaji akiwamo Elias Maguli mwenye mabao matano katika mechi saba, alisema “Ni mchezaji mzoefu kwa hiyo kuna kitu kaongeza ni vizuri kukutana na timu kubwa ukiwa na wachezaji wako waote,”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: